Unapokuwa kwenye mtandao wa Instagram unaacha kuscroll na kuweka “Attention” ya kutazama, kitu kinachofanya ufanye hivyo, mara nyingi ni kichwa cha habari ambacho kinaweza kikawa kimeandikwa katika picha, caption au kwa juu au chini ya video.
Kwahiyo leo utajifunza vichwa vya habari ambavyo ukitumia kwenye machapisho yako yaani maudhui ambayo unayaandaa kwa ajili ya wafuasi wako, utaweza kukamata attention yao na kuchukua hatua kwenye kile ambacho wewe unataka wafanye kupitia post yako, sekunde chache sasa utaanza kuwa mtu mwenye ushawishi kwa kutumia vichwa vya habari hivi, kazi yako itakuwa ni kukopi na kupaste
Vichwa vya habari 7 vinavyopendwa Mtandaoni
#1: Jinsi ya
Kwa aina hii ni lazima ujue matamanio yao, matataizo yao, maumivu yao, changamoto zao na wanafikiria nini kwa wewe kuwasaidia kupata kile wanachotaka kwa kuwakea kichwa cha habari jinsi ya kupata… (Taja) inasaidia mtu kusoma chapisho lako au kutazama video yako; kwa sababu watu wengi wanatafuta neno jinsi ya … yaani “How to…” kupata kile wanachotaka inaweza kua Instagram, Google, Facebook na Youtube.
Ni hivi mfano wewe ni mtaalamu wa mapishi unaweza kuacha kichwa cha habari “Jinsi ya kupika pilau tamu ndani ya dakika 30…!”, “Jinsi ya kupika pilau kuku…!, “Jinsi ya kupika keki tamu ya harusi kwa dakika 45 tu…!” n.k kwahiyo wewe unaweka kitu ambacho kitafanya mtu aache kuscroll na kusoma chapisho lako kwa kuandika kichwa cha habari kama hivi.
#2: Kwanini
Anza na neno kwanini maana inasaidia kukamata attention ya mtu kusoma chapisho lako na kuacha kuscroll na kutaka kujua sababu za wewe kusema kwanini kitu fulani kipo hivi au vile kwa mfano;
- Kwanini hutatengeneza pesa Instagram…?
- Kwanini hutopona maumivu ya kichwa ambayo yanakusumbua kwa muda mrefu…?
- Kwanini unahitaji sekunde 20 tu za kusikiliza podcast ya Mjasirimali digital…?
- Kwanini unashindwa kutimiza malengo yako ya mwaka 2023…?
- Kwanini unahitaji kujenga biashara imara mtandaoni…?
- Kwanini unashindwa kuuza bidhaa au huduma yako Instagram…?
SOMA: Je Uwe Influensa au Mfanyabiashara?
#3: Nilichojifunza
Unaandika kichwa cha habari kwa yale mambo ambayo umejifunza inaweza kuwa kwa kushindwa kwako, kufaulu au kufeli kwako, uzoefu ulioupata kwa kufanya kazi sehemu fulani, kwa kupata ujuzi wa aina fulani n.k kwahiyo watu wataka kujua umejifunza nini kwa mfano;
- Nilichojifunza kipindi na safari kwenda nchi mbalimbali duniani…!
- Nilichojifunza wakati nakuza ukurasa wangu wa Instagram.
- Nilichojifunza wakati napungua uzito wa kilo 15 ndani ya miezi minne…!
- Nilichojifunza wakati natumia mafuta ya XYZ ili kuwa na uso ambao hauna chunusi wala upele…!
- Nilichojifunza kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii…!
- Nilichojifunza namna ya kuingiza pesa Instagram bila ya kufanya matangazo ya kulipia…!
Watu wanataka kujifunza kupitia uhalisia wa mambo kwahiyo unawaambia ulichojifunza unateka usikivu wao na kutaka kujifunza kutoka kwako kwa yale ambayo umejifunza juu ya kitu au jambo fulani
#4: Sababu
Watu wanataka kujua sababu ya kitu ili wafanye baada ya kupata ukweli, taarifa kamili, uhakika na ushuhuda kuwa inawezekana na wao kupata matokeo kwa wewe kuanza na neno sababu ya …! Yaani “Reason to …!” inasaidia kuteka attention ya mtu na kusoma chapisho lako au kutazama video, kwa mfano unaandika
- Sababu 05 za kwanini unahitaji kupungua uzito…!
- Sababu ya kupoteza followers kila siku kwenye akaunti yako ya Instagram…!
- Sababu 04 za kwanini unapoteza nguvu ya ushawishi Instagram…!
SOMA: Idea 11 Za Reels Kuvutia Wafuasi Wapya
#5: Tumia namba
Watu wanaacha kuscroll kwa kuona namba juu ya kitu fulani huwa inakamata sana usikivu wao yaani “Attention” kwa mfano ,
- Jinsi ya kupungua uzito ndani ya siku 20…!
- Sababu 05 za kwanini uanze biashara mtandao wa Instagram…!
- Anza kutengeneza pesa mtandaoni ndani ya siku 21 baada ya kusoma kozi ya XYZ…!
- Anza kutumia kanuni ya dakika 02 kuishinda tabia ya kughairisha mambo…!
Anza kuweka namba kwenye vichwa vya habari yako ina nguvu sana maana watu wanapenda kupata matokeo ndani ya muda mfupi au kujifunza vitu vichache ili kupata muda wa kuendelea na mambo yao.
#6: Siri
Nani hapendi kuambiwa Siri? Hata mimi mwenyewe napenda siri aka ubuyu hahaha! Unacheka nakuona kabisa mtaalamu , kwahiyo acha kuweka focus tu kuweka mapicha tu utapoteza nguvu ya ushawishi kwenye mitandao ya kijamii, kwa mfano;
- Siri ya kuuza keki Instagram…!
- Siri 04 za kuvaa na kupendeza …!
- Siri 05 za kupika chakula kitamu nyumbani kwako…!
- Siri 06 za kutengeneza video qulity za mauzo kwenye mitandao ya kijamii…!
- Siri ya kuwa na ngozi nyororo kama yangu…!
Hebu funguka kwa kuwafichulia watu siri na utaweza kuona matokeo makubwa kwenye kitu unachofanya ni wewe kwenye kichwa chako kuanza na neno siri kisha unaweka mada then boom…!
#7: Neno “yako”
Ukitumia neno yako kwenye kichwa chako cha habari inamfanya mtu aone upo kwa ajili yake na unaelewa maumivu yake, changamoto zake, matatatizo yake, anafikiria ni nini na matamanio yake kwa sababu watu hawajali kabisa kuhusu wewe bali wanajali sana kuhusu wao kwahiyo kutumia neno “Yako” inamfanya mtu aache kuscroll na kusoma au kutazama video yako na acha kutumia neno “Yangu” itafanya uonekane mbinafsi.
Kwa mfano,
- Kwanini unapaswa kukuza biashara yako…?
- Kwanini ngozi yako ina chunusi na madoa…?
- Sababu 05 za kwanini unaweza kutimiza malengo yako kwa kishindo…!
- Jinsi ya kuacha tabia ya kujilinganisha ili uwe na amani ya moyo na furaha kwenye maisha yako…!
Anza sasa kutumia neno “Yako” kwene kichwa cha habari yako na utakuja kunipa ushuhuda namna gani machapisho yako yanafanya vizuri au video zako kupata watazamaji wengi.
Sikiliza podcast hapa
Hitimisho
Asilimia 80% watu wanasoma vichwa vya habari kwanza kabla ya kusoma chapisho au kutazama video kwa maana hiyo tumia vichwa hivi saba kwenye machapisho na video zako itafanya upate “Engagement” kubwa na post zako kufanya vizuri.
Je, umejua jinsi ya kuandika vichwa vya habari ambavyo vinateka attention ya watu mtandaoni? Acha maoni yako hapo chini.
Endelea kufuatilia Mjasiriamali Digital kupata dondoo makini sana za kuongeza wafuasi na mauzo kwa ajili ya biashara yako katika jukwaa la instagram.