Katika makala hii tunaenda kuchambua stika 10 zinazoongeza engagement kwenye Instagram stories. Bila shaka utakuwa umeshagundua kuwa stories huwa kuna wakati zina views nyingi kupita hata posti za kawaida.
Hiki ni kiashiria kikubwa kwamba kuna nafasi kubwa sana ya kufaya mauzo zaidi na kupata wafuasi kama utakuwa makini katika kutumia mbinu za kuposti Instagram stories badala ya kuposti tu bila malengo.
Engagement ni nini?
Engagement ni kipimo cha jinsi watu wanavyofurahishwa au kufaidishwa na posti zako kwa kuangalia idadi ya Likes, komenti, shares, idadi ya watu wanaosave posti zako nk.
Engagement kubwa (nzuri) Maana yake akaunti inapata Like, comments,saves, shares nyingi ukilinganisha na idadi ya wafuasi wake. Engagement ndogo (mbaya) maana yake akaunti ina followers(wafuasi) wengi lakini likes, comment, saves na shares ni chache.
Engagement ni kitu muhimu sana Instagram kwasababu, zile akaunti ambazo zina engagement kubwa ndizo ambazo Instagram huzipromote zikue zaidi kwa kuonesha posti zao kwa watu wengi zaidi.
Hii inamaanisha kuwa ukitaka kupata wafuasi wengi zaidi unapaswa kufanya mbinu za muhimu sana kuhakikisha unawafanya watu wengi zaidi angalau wa LIKE na ku KOMENTI kwa wingi kwenye posti zako. Mfano wa mbinu hizi ni kutumia hizi stika 10 zinazoongeza engagement kwenye Instagram stories.
STIKA ZINASAIDIAJE KUONGEZA ENGAGEMENT?
Ninatumaini kuwa umeshaziona na umeshawahi kutumia stika mbali mbali ambazo zinapatikana kweye kipengele cha Instagram stories.
Watu wengi huzitumia hizi kama urembo lakini kwa wafanyabiashara hizi ni nyenzo muhimu sana kwa kuongeza wafuasi na mauzo kwa kupitia kuongeza engagement.
Unapotumia stika tunazoenda kuzijadili katika makala hii, utaona kuwa instagram stories zako zitaanza kupata views nyingi zaidi na watu wengi zaidi wataaacha ujumbe kwenye DM yako.
STIKA 10 ZINAZOONGEZA ENGAGEMENT INSTAGRAM STORY
#1: Stika ya “Sound On”
Watu wengi huwa wanaangalia instagram stories bila sauti.Hii inaweza kuwa inasababishwa na labda mtu kuwa hana headphones zake karibu huku yupo mbele za watu.
Lakini pia watu wengi hujisahau kubonyeza screen ili sauti ije, na wengine hawajui jinsi ya kufanya sauti isikike.
Kama instagram story yako ina muziki mzuri au kama ina ujumbe wa sauti basi stika hii itamfanya mtu abonyeze na asikie sauti ili asipitwe na ujumbe.
Kile kitendo cha mtu kubonyeza ile stika kunaonesha Instagram kuwa akaunti yako ina ushawishi wa hali ya juu kwasababu watu wengi wanaonesha ushirikiano kwa kuboneza kitu ulichoweka.
Hii italeta uwezekano mkubwa zaidi wa wao kuionesha hii stori kwa watu wengi zaidi hivyo kukuongezea views.
JINSI YA KUWEKA STIKA HII KWENYE INSTA STORY
- Bonyeza kitufe cha stika (Sehemu ya juu ya screen ni kitufe chenye umbo la kibox chenye macho na tabasamu).
- Kwenye sehemu ya kusearch andika “Sound on” na stika itatokea. Au bila kusearch unaweza kushuka chini na kuangalia stika moja moja hadi ukutane na ya sound on.
- Ibonyeze stika na itatokea kwenye instagram stori yako.
#2: Stika ya “Support Small Business”
Kama tulivyochambua jinsi ya kuongeza wafuasi na mauzo kwa kufanya collabo na wafanyabiashara wengine katika makala iliyopita (BONYEZA HAPA KUSOMA), Stika hii ni muhimu sana katika kutimiza mbinu hii kwa haraka zaidi.
Unachotakiwa kufanya ni kutafuta mfanyabiashara ambaye maudhui yenu yanafanana lakini bidhaa zenu hazifanani.
Kisha ongea naye kuhusu jinsi wafuasi wako wanavyoweza kufaidika na biashara yake na vivyo hivyo wafuasi wake wanavyoweza kufaidika na za kwako.
Baada ya hapo mnaweza kukubaliana kufanyiana promotion kwa kutumia stika hii ya “Support Small business”.
Kitakachotokea utakapotumia stika hii ni kwamba utaweka jina la akaunti ya biashara unayotaka wafuasi wako wafaidike nayo.
Watu wako watakapoona story yako na kubonyeza kitufe cha stika hii basi wataweza kuona baadhi ya posti za akaunti hiyo unayoipromote.
Pia wataweza kuitembelea kiurahisi kabisa kwa kubonyeza jina akaunti hiyo kwenye stika.
FAIDA ZA STIKA YA “SUPPORT SMALL BUSINESS”
- Engagement itaongezeka kwasababu watu lazima watabonyeza tu ili kuona bidhaa za hiyo akaunti nyingine uliyoipromote.
- Wafuasi watakufurahia kwa kuwa unaonesha kusapoti wafanya biashara wenzako. Pia utakuwa unaonesha kuwajali kwa kuwaunganisha na bidhaa nyingine nzuri ambazo wanaweza kuwa wanazihitaji.
- Yule utakayempromote na yeye atakupromote kwa hiyo utapata wafuasi na wateja wapya kutoka kwake!
JINSI YA KUWEKA STIKA HII KWENYE INSTA STORY
- Ukishaupload instagram story yako nenda kwenye kipengele cha stika na usearch “Support small business”.
- Ukiibonyeza stika utaelekezwa uweke jina la akaunti ya instagram ya biashara unayotaka kuipromote. Acha muundo kama ulivyo hauna shida ya kuedit wala kufanya mabadiliko yoyote.
- Post stori yako.
#3: Stika ya ‘Quiz’
Hii ni stika ambayo inakuwezesha kuuliza swali na kupata majibu kupitia instagram stories.
Katika hizi stika 10 zinazoongeza engagement hii inaongeza sana kwasababu watu wengi watajibu maswali lakini pia watarudi tena ili kupata mtazamo wako juu ya majibu yao.
- Nenda kwenye kipengele cha stickers na u search “Quiz”
- Weka swali unalotaka kuuliza pamoja na chaguo la majibu yaani A,B,C,D nk.
- Usisahau kuashiria chaguo lipi ndio sahihi ili watu wakilichagua hilo litokee kwa rangi ya kijani kuashiria kuwa wamepata. Na wale watakaochagua tofauti itatokea rangi nyekundu kuashiria kuwa wamekosea.
- Kama unataka kubadilisha rangi ya boxi lako la quiz basi bonyeza alama ya duara lenye rangi iliyopo juu kabisa ya screen. Zitatokea rangi nyingi na utaweza kuchagua moja inayendana na brand yako.
Stika hii ni nzuri kwa ajili ya kuelimisha na kuchangamsha wafuasi wako.
Lakini pia ni nzuri sana kwa kufanya tafiti ambazo zitafaidisha biashara yako kwa kuwauliza maswali yanayoendana na bidhaa au huduma zako.
#4: Stika ya Poll
Hii ni aina nyingine ya stika ambayo itaongeza engagement yako maradufu kwasababu huwa na swali rahisi na haraka kujibu.
Stika hii inafanya watazamaji kuchagua moja kati ya mambo mawili tu.Lengo kubwa ni kwa wewe kufahamu vitu ambavyo wanapendelea zaidi ili iwe rahisi kuona kama biashara au huduma yako inaweza kuwapatia vitu hivyo.
JINSI YA KUWEKA STIKA HII KWENYE INSTA STORY
- Nenda kwenye kipengele cha stika na usearch “Poll”
- Ukiibonyeza stika utaona sehemu ya “Ask a question” ambapo unaweza kuandika swali kisha kwenye vibox ukaweka “NDIO” au “HAPANA”
- Au unaweza kuacha sehemu ya “Ask a question” wazi, kisha kuweka machaguo yako mawili kwenye vibox badala ya “NDIO” na “HAPANA”
Kwa mfano Swali linaweza kuwa “Team iphone forever?” chaguo likawa NDIO na HAPANA.
Hapa wenye iphone watachagua ndio na wasiotumia watachagua hapana.
Kama biashara yako ni kuuza simu na vifaa vyake utaweza kujua wafuasi wako wanatumia aina ipi zaidi hivyo kukusaidia katika kufanya maamuzi sahihi wakati unaongeza bidhaa.
Mfano wa Pili ni kuacha sehemu ya swali wazi na kuandika tu majibu kwenye mabox
- Box 1: Team Iphone for life
- Box 2: Team android for life
Hapa wenye iphone watachagua box lao na wenye Android watachagua lao.
Mwisho utapata kufahamu ni asilimia ngapi wanatumia aina ipi na asilimia ngapi wanatumia nyingine.
Watakaopiga kura pia wataweza kuona papo hapo kuwa asilimia ngapi ya watu waliojibu wanatumia aina ipi ya simu.
#5: Stika ya Questions
Hii ni stika nzuri sana ya kupata maoni kutoka kwa wafuasi wako kwa kuwahamasiha kukuuliza wewe swali au wewe kuwauliza wao swali.
Unapotumia hii, wafuasi wako wataona kuwa unajali kuwatatulia matatizo yao na unapenda kuwasiliana nao na kupata mitazamo yao.
JINSI YA KUWEKA STIKA HII KWENYE INSTA STORY
- Nenda kwenye kipengele cha stika na usearch “Questions”
- Ukiibonyeza stika utaona sehemu ya “Ask me a question” ambapo unaweza kuandika kitu cha kuhamasisha mtu aulize swali. Mfano unaweza andika “Tunajali mchango wako, karibu tuulize swali lolote”. Au swali lolote lile kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu.
- Kipengele cha “ Viewers respond here” unakiacha maana hapo ndipo watu wataandika maswali.
- Mtu yeyote akiandika swali litakuja moja kwa moja kwenye DM yako.
#6: Stika ya “Hashtag”
Stika hii husaidia kuongeza engagement kwa njia mbili.
Kwanza: Watu wengi watabonyeza ili waweze kuangalia posti nyingine nyingi za watu wengine ambazo zina hashtag hiyo.
Pili: Posti zote zenye hashtag moja huwa zinaenda kukaa kwenye ukurasa maalumu wa hashtag hiyo. Hii huleta uwezekano mkubwa wa watu wapya kuona posti yako, kufurahishwa nayo na kuku-follow kwa ajili ya kuona zaidi.
JINSI YA KUWEKA STIKA HII KWENYE INSTA STORY
- Nenda kwenye kipengele cha stika na usearch “Hashtag”
- Ukiibonyeza stika utaweza kuandika hashtag inayoendana na maudhui ya posti yako.
- Ukishaiweka kwenye posti yako unaweza kubadilisha muonekano wake kwa kuibonyeza stika hiyo mara nyingi hadi itokee katika ule muonekano unaoupenda.Unaweza kuweka stika hii moja tu kwa kila posti moja.
#7: Stika ya @Mention
Hii ni stika ambayo kazi yake ni kutaja mtu au akaunti nyingine ya Instagram ambayo inatokea kwenye posti uliyoiweka.
Kwa mfano una hoteli na ukapiga picha watu ambao majina yao ya instagram unayafahamu, utakapoposti picha na kutumia stika hii utaweza kuwataja akaunti zao hivyo kupelekea watu watakaoona stori waweze kuwafahamu na kuweza kutembelea kurasa zao.
Watu wote wanaotajwa kwa kutumia stika hii hupata ujumbe kuwa umeposti kitu kinachowahusu kwenye stori yako.
Hii mara nyingi sana hupelekea wao kuipost hii stori yako wenye story zao pia ili kuonesha wafuasi wao kuwa biashara yako imewafurahia na kuwa post. Hivyo kupelekea uwezekano wa wewe kupata wafuasi wapya kutoka kwenye akaunti zao.
Mara nyingi sana wafuasi wako watabonyeza hizi stika na kuangalia akaunti za watu wote uliowataja kwa kutumia stika hii.
Hii huwaonesha kuwa kwanza biashara yako ni ya ukweli na ina wateja waukweli. Pia itaonesha kuwa unawajali na unawafurahia wateja wako hadi kufikia kuwapost na kuwatag.
JINSI YA KUWEKA STIKA HII KWENYE INSTA STORY
- Nenda kwenye kipengele cha stika na usearch “@mention”
- Ukiibonyeza stika utaweza kuandika username au jina la akaunti ya instagram unayotaka kuitaja.
- Kama katika stika ya Hashtag, hii nayo unaweza kubadilisha muonekano kwa kuibonyeza hadi kufikia ule utakaokupendeza. Lakini tofauti na stika ya Hashtag, unaweza kuweka stika hii zaidi ya moja kwenye stori moja.
#8: Stika ya “Location”
Ukilinganisha na hizi stika 10 zinazoongeza engagement Instagram stories, hii inaongeza engagement kidogo kwasababu mara nyingi huwa watu hawana sababu ya kuibonyeza.
Badala yake stika hii itasaidia kuongeza uwezekano wa kupata wafuasi wengi zaidi hasa wa kutoka maeneo ya karibu na eneo lililowekwa kwenye location.
Yaani kwa mfano umeweka location ya Mikocheni, Dar es salaam. Watu wengi zaidi wa mikocheni na DSM kwa ujumla watakuwa na uwezekano wa kuoneshwa posti yako.
Kwenye sehemu ya stickers search “location” au utaiona tu ukishuka chini. Kisha anza kuandika location ulipo na automatically instagram itaanza kukupa maeneo ya karibu uchague.
Kama kawaida ukibonyeza stika muonekano utabadilika hadi ufikie unaoutaka.
#9: Stika ya “GIF”
Gif ni aina ya stika za video fupi sana ambazo hujirudia rudia. Lengo la stika za gif ni
- Kuongeza mvuto wa posti.
- Kuburudisha au kuchekesha
- Kutilia mkazo stika inayohitaji mtu abonyeze au aandike kitu. Kwa mfano unaweza kutumia gif yenye mishale ielekee kwenye box la maswali ili mtu ajue kwamba ni anatakiwa kujibu.
Wafuasi wako watapendelea sana na hawatakosa kuangalia stories zako mpya kwasababu watakuwa wanavutiwa na gif mbali mbali unazoziweka.
Unaweza kuweka stika ya Gif kwa kubonyeza sehemu ya stickers na kuchagua au ku-search “Gif”.
Hapa instagram italeta gif nyingi sana ili uchague moja. Kwa kuokoa muda unaweza ku-search aina ya gif unayotaka na zitatokea nyingi za kuchagua.
Ukipata unayoipenda na ukaibonyeza itatokea kwenye stori yako. Kama imekaa eneo ambalo si zuri au kama inaficha kitu muhimu basi unaweza kuihamisha kwa kuishikilia kisha kuisogeza kwenye eneo inapohitajika.
#10: Stika ya “Countdown”
Hii ni stika ambayo inaonesha ni muda gani umebaki kwa kabla ya kitu au tukio fulani kuanza au kuisha kwa mfano.
- Bidhaa mpya kufika: Kama unafahamu kuwa bidhaa mpya zitaanza kuuzwa siku fulani basi ni vizuri kuweka tangazo kwenye posti za kawaida kuwakumbusha wateja. Pia ni muhimu kuweka countdown kwenye stories ili kuendelea kuwakumbusha muda unapokaribia.
- Punguzo la bei: Kama umeamua kufanya SALE maalumu kwa ajili ya tukio fulani ambalo linaisha ndani ya muda mfupi. Stori yenye countdown itahamasisha zaidi watu kuwahi tukio kabla halijaisha.
- Mwisho wa shindano: Stika ya countdown ni muhimu sana pale unapokuwa una host shindano au giveaway. Watu hawataweza kulalamika kuwa hawakujua muda wa kushiriki umepita kama utakumbuka kupost stika hii.
Unaweza kuweka stika ya countdown kwenye instagram stori yako kwa kubonyeza kwenye kitufe cha stickers na kusearch “Countdown”.
Stika ikitokea ibonyeze na ujaze sehemu zifuatazo. Kwenye “Countdown name” weka jina la tukio. Mfano unaweza kuweka “Mwisho wa punguzo la Christmass”.
Jaza tarehe na muda wa tukio kuisha au kuanza na utakuwa umemaliza.
Kama kawaida kila ukibonyeza stika muonekano utabadilika hadi ufikie unaoutaka.
FAIDA KUU YA STIKA YA COUNTDOWN
Stika inampa mtazamaji chaguo la kukumbushwa kabla tukio kuisha, au kukumbushwa tukio linapoanza ili asichelewe.
Yaani kama ountdown yako inahesabu muda uliobaki kabla ya bidhaa mpya kuingia dukani. Basi mteja wako anaweza kufanya instagram imtumie ujumbe pale muda utakapokaribia ili nayeye aweze kuwahi bidhaa kabla watu wengine hawajazimaliza.
Kwa kifupi
Ni rahisi sana kwa wafanyabiashara kuamua kuposti tu bila kutumia mbinu kama hizi za mafanikio. Hii mara nyingi hutokana na aidha kuwa na mambo mengi ya kufanya, uvivu au kutojua vitu vya kufanya.
Hizi stika 10 zinazoongeza engagement wala hazichukui hata zaidi ya dakika tano kuziweka kwenye instagram stori zako.
Manufaa ya kuzitumia ni makubwa sana ukilinganisha na muda mchache wa kuziweka.
Ukweli ni kwamba ingawa mbinu zipo za kufanikiwa Instagram, wafanyabiashara wengi huwa hawazitumii.
Kuwa wa tofauti, jifunze kupitia Mjasiriamali Digital. Kila siku utakuta aidha makala mpya hapa kwenye website, au podcast mpya au post moto kabisa instagram za kukupa mbinu madhubuti za kukuza biashara yako kwa kuptitia jukwaa la Instagram.
Kama muda ni changamoto hakiharibiki kitu!. Wasiliana na mimi niweze kukufundisha au kukuendeshea akaunti yako ya biashara kwa mbinu za kisasa!
Mwisho kabisa, jaribu kutumia stika hizi na ushuhudie jinsi utakavyopata mafanikio kupitia kukua kwa engagement yako!.