Kama wewe ni mtengeneza maudhui instagram au unafanya biashara kwenye mtandao wa instagram, kupata wafuasi wa maana ni jambo la msingi ili kuhakikisha unafaidika na unachokifanya,
Wafuasi wa maana ni wapi? Wafuasi wa maana ni wale ambao walikuwa wanatafuta utatuzi wa matatizo waliokuwa nayo na walio tayari kuwekeza kwenye bidhaa au huduma yako na sio kuwa na wafuasi mradi. Je unajua kwanini unapata wafuasi mradi na wasio tayari kununua kwako au kufanya biashara na wewe? Hizi ni sababu 6 kwanini haupati wafuasi wa maana Instagram.
Sababu 6 kwanini haupati wafuasi wa maana
1. Haujui unazungumza na nani kwenye akaunti yako
Kama katika ukurasa wako wa instagram unazungumzia kila kitu kinachokuja akilini mwako mara leo wewe ni mshauri wa mahusiano, crypto currency, utapost biashara ya matikiti, ujakaa sawa kesho ni mtu wa masuala ya dini, Jioni hatujapumua umekwazana na mtu umeanza kuchambana kwenye ukurasa wako wa kibiashara, kwa hali hiyo na haitakuelea watu ambao watakusikiliza na kuchukua hatua juu ya kile unachokifanya.
Ufanye nini sasa? Kaa chini jipambanue wewe na jiulize unataka kutambulika kama nani kwenye kurasa zako za biashara ukizingatia kwa makini ujuzi, maarifa, watu unaotamani kufanya kazi nao, vitu unavyopenda na vipaji vyako. Kama ukisema ‘’Nasaidia watu kupunguza uzito watu bila kufanya mazoezi magumu’’ bado hutaweza kudaka soko lako kwa haraka, hivyo basi wasifu wa ukurasa wako utuambie walengwa wako zaidi mfano ‘’Nasaidia akina mama waliojifungua kupunguza kilo 10 ndani ya siku 30 bila mazoezi’’ tayari hapo utaweza kupata akina mama na kuwauzia program zako na bidhaa.
2. Maudhui yako hayaendani na wasifu wako
Kama kwenye bio yako umeandika wewe ni mtaalamu wa mazoezi kwa akina mama, basi maudhui unayochapisha yanatakiwa yawe yanawagusa walengwa wako. Unaweza kuchapisha video za mazoezi, vyakula, hamasa ya kila siku kwa ajili ya watu wako, shuhuda za watu waliofaidika na bidhaa au huduma yako, maudhui ya kujitangaza kama una ofa au mzigo mpya pamoja na kutuambia kwanini wewe ni chaguo sahihi kwetu. Ukifanya hivyo utabadilisha biashara au kile unachokifanya kwenye ukurasa wako wa Instagram na kupata wafuasi potential
3. Hauchapishi mara kwa mara
Kwenye mitandao ya kijamii haupo peke yako unayehitaji kundi hilo la watu unaowalenga, la hasha kuna watu wengine zaidi, Hivyo basi kuonekana mara kwa mara mfano kwa wiki mara 3 au kila siku utajiweka akilini mwa walengwa wako tofauti na mshindani wako ambaye anapest mara moja kwa mwezi. Ukiwa na mkakati sahihi wa hicho unachokifanya utajua nguzo ya maudhui yako na kufahamu uchapishe nini na kwa wakati gani kwenye ukurasa wako na kuendelea kufanya kwa muendelezo.
4. Ukurasa wako ni mchafu na hauna mashiko
Katika hatua za kutafuta ni wapi pa kula au pa kulala ukiwa unasafiri au kutoka out na marafiki, mara nyingi tunaingia instagram kuangalia mgahawa ulio karibu na tunatazama kwenye kurasa mbalimbali tukiangalia muonekano wake kwenye picha, picha na video za vyakula, bei zao, inafungwa saa ngapi na umbali kutoka nilipo, huduma nyingine nzuri kwa wateja wao na mengine zaidi.
Sasa kama ukurasa wako hauleweki unazungumza na nani na unamvutia nani itakuwa ngumu kutushawishi kuja au kununua kwako. Mfano kuna migahawa ipo barabarani na ni nzuri kwa watu ambao hawatakaa kwa muda mrefu na mingine ni migahawa iliyo kwenye sehemu tulivu ambayo unaweza kukaa na mtu kwa ajili ya kikao. Kwahiyo ukurasa wako utupe picha hiyo kulingana na watu unaowalenga
5. Unafanya mikakati iliyopitwa na wakati na kuharibu chapa yako mtandaoni
Nilianza kutumia mtandao wa instagram mwaka 2012 kwa kipindi hicho ilikua kuna lile suala ya kwamba kuwa na wafuasi wengi au likes unaonekana ni wa thamani katika kundi la marafiki zako au watu wanaokuzunguka. Inaniuma sana kuona mfanyabiashara kuumiza kichwa kwa idadi ya wafuasi alionao badala ya kuwaza ni idadi ngapi ya simu za wateja umepokea na ni wangapi wamegeuka kuwa wateja.
Anaenda mbele zaidi na kufanya mikakati iliyopitwa na wakati kam kununua fake followers, likes, views, comments, follow/unfollow, like 4 like na wakati bidhaa zimemdodea ndani anaishia na hakuna miamala yoyote inayoingia ili kuboresha maisha na biashara yake.
6. Kutotumia matangazo ya kulipia(Facebook Ads)
Kama unafanya biashara na haufanyi matangazo ili upate maulizo au mauzo ya bidhaa au huduma yako biashara yako inakaribia kufa kabisa, wewe ni shahidi tuna makampuni makubwa ya mitandao ya simu na kila kukicha tuanona yafanya matangazo mtandaoni na redioni au kwenye televisheni kusambaza habari njema kuhusu huduma na bidhaa zao. Sijamaanisha ukimbie kwenye televisheni ila kuna mbdala amabyo ni mzuri kwa biashara yako ndogo, yanaiitwa Facebook na Instagram ads ambayo yanakupa nafasi ya kuonekana kwa watu ambao walikuwa hawafahamu kuhusu brandi au biashara yako.
Mafanikio ya matangazo haya nategemea na malengo yako kwenye biashara, kuna baadhi ya wafanyabiashara hufanya matangazo ili wapigiwe simu au watumiwe ujumbe mfupi kwenye whatsapp, facebook au instagram, wengine wanataka watu watembelee tovuti au kurasa zao na kuzifuata(follow). Kuna njia nyingi ya kufanikisha urushaji wa tangazo lako, njia ya kwanza ni kujifunza na kufanya mwenywe au kumtafuta mtaalamu ukusetie kila kitu wewe ukae kusubiria matokeo yake Sababu 3 kwanini utumie facebook ads 2022
Na imani umejifunza kitu kikubwa kwenye makala hii ya sababu 6 kwanini haupati wafuasi wa maana instagram , Share makala hii kwenye kikundi cha whatsapp, telegram, twitter au facebook ili wafanyabiashara na wajasiriamali kama wewe waje wajifunze!