Amani Longishu

Sababu 3 kwanini utumie facebook ads 2022

Sababu 3 kwanini utumie facebook ads 2022

Table of Contents

Sababu zipo nyingi kwanini uanze kutumia matangazo ya kulipia ya facebok kwa ajili ya biashara yako ya biadhaa au huduma. Kwenye makala hii nimekuandalia sababu 3 kwanini matangazo hayo ni muhimu kwako!

1. Ni nafuu tofauti na mitandao mingine

Ukizungumzia suala la unafuu wa bei ya matangazo, facebook imekuwa chanzo cha kufanikisha biashara za watu wengi hasa wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo. Kwa kiasi cha $2(Tsh 4650) kwa siku unaweza kuanza kurusha matangazo na watu wakaona na kukupigia simu, kukutumia ujumbe mfupi au hata kutembelea tovuti ya biashara yako.

2. Watu unaowatafuta wanapatikana facebook pia

Kama ulikua haufahamu, kwa siku watu wanatumia dakika 40 hadi saa 3 kwenye mtandao wa kijamii mmoja hivyo basi, facebook ni sehemu sahihi ya kujionyesha wewe ni nanii, unafanya nini na watu wanaweza kufaidika na wewe kwa namna gani, hata pia kutangaza bidhaa au huduma zako.

3. Unaweza kuwalenga watu wa aina fulani

Raha ya kufanya matangazo ni waone watu sahihi ambao wanaweza kuwa wanahitaji huduma au bidhaa kama yako, Kwahiyo kupitia facebook unaweza kuwalenga watu wenye umri na jinsia fulani, wanaopataikana mikoa au nchi fulani, wanaotembelea kurasa fulani mtandaoni au wanaosheherekea sikukuu ya kuzaliwa mwezi fulani au wenye tabia fulani wakiwa mtandaoni mfano wanaopenda kutazama video za mapishi au vichekesho na mengineyo.

Je umejifunza? utaanza kutumia matangazo ya facebook katika kukuza na kusambaza habari njema kuhusu bidhaa au huduma zako? Niandikie maoni yako nitayasoma na kujibu hapo chini.

Share Makala Hii Kwa Wengine

Pata Kitabu

Hatua kwa hatua jinsi ya kuuza bidhaa online bila duka wala ofisi

Pata Kitabu

Pata copy yako leo uanze kutengeneza pesa kwenye Instagram

ZINAZOTREND