Amani Longishu

Jinsi ya kupata Followers wengi instagram kwa kufanya collabo

Jinsi ya kupata followers wengi kwa kufanya collabo

Table of Contents

Je, una akaunti ya instagram kwa ajili ya biashara yako na ungependa kufahamu jinsi ya kupata wafuasi wengi zaidi ili kuongeza mauzo?. Kama jibu ni ndio basi hii makala ni special kwa ajili yako!

Watu wengi sana hudhani kuwa njia pekee ya kupata wafuasi wengi zaidi Instagram ni kupitia kulipa matangazo ya biashara.

Hii huwa inakatisha tamaa hasa wale ambao biashara zao ni mpya kidogo na hawana bajeti kubwa ya kulipia matangazo.

Ukweli ni kwamba unaweza kupata wafuasi wengi zaidi Instagram na kuongeza idadi ya mauzo yako ya siku kwa kupitia mbinu hizi 2 ambazo unaenda kuizona katika makala hii.

Njia ya bure kabisa ya kupata wafuasi wengi na mauzo zaidi ni kupitia ushirikiano na wafanyabiashara wengine. Kwa lugha rahisi tunaweza kusema “Kufanya collabo”.

Lengo kuu la kufanya collaborations kati ya wafanyabiashara ni kubadilishana wale wafuasi wenu. Kama wewe una wafuasi 1000 na mwenzako anao 1,000 basi wewe utapata watu wapya kutoka kwake na yeye atapata wapya kutoka kwako.

JINSI YA KUPATA WAFANYABIASHARA WA KUFANYA NAO COLLABO

Chagua siku ambayo umetulia na uingie kwenye sehemu ya “search” katika Instagram yako. Kisha anza kuandika maneno ambayo hutumiwa sana kwenye maudhui ya biashara unazotafuta kufanya nazo collabs.

Ukishawapata ni vizuri kuandika majina ya akaunti zao kwenye notebook yako pembeni kisha kuwatumia ujumbe DM.

Kama DM haitajibiwa kwa wakati basi unaweza kuchukua hatua inayofuata ambayo ni kuwatumia ujumbe wa simu.

Mara nyingi wafanyabiashara huwa wanaweka namba zao za simu kwenye profile zao ili kurahisisha mawasiliano na wateja.

Ni vizuri zaidi kama utaanza na ujumbe kabla ya kupiga simu. Hii ni kwasababu katika ujumbe hasa kupitia WhatsApp utaweza kutuma link ya akaunti yako ya biashara ili mlengwa aweze kupitia na kuona kama kweli itamfaidisha kushirikiana na wewe.

Baada ya hapa mnaweza kuanza kuongea na kupanga hatua zinazoendelea.

VITU VYA KUZINGATIA UNAPOCHAGUA MTU WA KUFANYA NAYE COLLABO.

Aina Ya Bidhaa

Mbinu ya muhimu kabisa ya kuhakikisha unapata wafuasi wengi zaidi kwa kupitia collabs ni kuhakikisha una collabo na wafanyabiashara ambao bidhaa zao zinaendana na za kwao.

Usifanye collabo na wale ambao bidhaa zenu zinafanana kabisa kwasababu utakuwa unajenga mazingira ya ushindani.

Kwa mfano wewe unauza Lishe ya watoto, haitakiwi ukafanye collabo na mjasiriamali mwengine anayeuza unga wa lishe, wala yule anayeuza nafaka ambazo zinaweza kutengenezea lishe.

Hii ni kwasababu ni rahisi kwa wateja kumchagua mmoja na kutonunua kwa mwengine.

Lakini kama wewe unauza unga wa lishe na ukafanya collabo labda na mtu anayeuza nguo za watoto au vifaa vya kuchezea vya watoto, itakuwa na manufaa zaidi kwasababu wateja wenu ni wa aina moja yaani wazazi.

Wateja wa yule muuza nguo na midoli watageuka kuwa wateja wa lishe yako na wateja wako watageuka kuwa wa wateja wa nguo na midoli kwa yule uliyefanya collabo naye.

Idadi Ya Wafuasi

Ili kufanikiwa katika suala zima la jinsi ya kupata wafuasi wengi wa Insatgram kupitia kufanya collabo ni muhimu sana kuwa makini na kiasi cha followers/wafuasi wa mtu unayetaka kufanya nayeushirikiano.

Watu wengi hudhani kuwa yapo manufaa zaidi kama watafanya collabo na biashara ambazo zina wafuasi au followers wengi sana zaidi yao. 

Hii si kweli kutokana na sababu zifuatazo:

  1. Followers feki: Unaweza kukuta profile ina followers laki mbili kumbe wa ukweli ni 500 tu. Hapa collab itamfaidisha yeye zaidi kuliko wewe.
  2. Kulipishwa huduma: kama idadi ya wafuasi wako ni ndogo sana kupita wao basi kuna uwezekano mkubwa sana wakakuambia ulipie collabo kwasababu itaonekana kama wewe ndio utafaidika kuliko wao.
  3. Kukataliwa kabisa: Mara nyingi akaunti zenye wafuasi wengi zaidi huwa hawapendelei collabo na akaunti ndogo. Wakati mwingine pia ni kwasababu huwa wanapata DM nyingi sana kwa hiyo ya kwako inaweza kuwapita au kuonekana kama haina umuhimu sana. Au pia wanaweza kuwa na mauzo mengi sana kiasi kwamba hawahitaji kufanya collabs ili kuongeza wafuasi na kupata mauzo zaidi. 

Wakati wa kufanya uchunguzi juu ya wafanyabiashara wa kushirikiana nao ni vizuri zaidi kutafuta wale ambao maudhui yenu yanaendana, bidhaa zenu hazifanani 100%, na pia wale ambao wana idadi ndogo au ya saizi ya kati ya wafuasi ambao huwa wana Like na kucomment mara kwa mara kwenye posti zao.

JINSI YA KUPATA WAFUASI WENGI INSTAGRAM KUPITIA COLLABO.

Sasa ukishapata partner wako wa collaboration na mkishakubaliana bidhaa zipi za kupromote mnatakiwa sasa kuchagua njia ya kufanya collabo yenu.

Zipo njia mbili ambazo zinapendwa zaidi katika suala hili la collaborations za instagram kama unavyoenda kuziona sasa.

#1: Kutengeneza collab za Instagram posti au Reels.

Instagram imeongeza teknolojia mpya katika kipengele cha kuweka posti za kawaida na reels kinachoitwa ‘Instagram collab feature‘.

Kwa kutumia hiki unao uwezo wa kukaribisha mtu mwingine au akaunti nyingine ionekane na itajwe kama mchangiaji katika kutengeneza posti au reel ambayo unaiupload.

Hapo mwanzo kulikuwa na njia mbili za kuonesha wafuasi kuwa posti fulani imetengenezwa kwa ushirikiano kati ya akaunti mbili.

Njia ya kwanza ni kupitia ku TAG hiyo akaunti ambayo unafanya nayo collabo. Na njia ya pili ni kwa kupitia kipengele cha BRANDED CONTENT ambacho hutumika pale ambapo mtu amelipwa na akaunti nyingine kuweka post fulani.

Katika branded content pale kwenye post itatokea taarifa ya “Paid partnership with” na jina la akaunti iliyoilipia posti ile ipostiwe.

Jinsi ya kupata wafuasi instagram

Njia hii ilikuwa nzuri zaidi ya kutag kwasababu angalau majina ya akaunti zote mbili yanatokea juu ya post. Hii inakuwa rahisi kwa watu watakaoona post kwenda kwa ile akaunti nyingine iliyotajwa kuangalia bidhaa zaidi.

Lakini katika collabo hizi za kushirikiana huwa hakuna malipo. Kwa hiyo ndio maana Instagram ikaamua kutengeneza njia nyingine (Instagram collab feauture) ili kusaidia watu ambao hawafanyi collab za kulipana bali za kushirikiana wafuasi tu.

 JINSI YA KUTENGENEZA COLLAB KWA  Instagram Collab Feature

Anza kama unavyokuwa unanza kuposti picha, video au reel. Ukifika kwenye sehemu ya kushare chagua “Tag people” kisha bonyeza

“Invite Collaborator. 

Katika sehemu ya kukaribisha mshiriki (Invite collaborator tab) tafuta jina la akaunti ya biashara ambayo una makubaliano nayo ya collab. Ukiandika jina lao, akaunti ya itatokea na utaibonyeza. Mpaka sasa unaweza kushirikiana na akaunti moja tu.

Jinsi ya kupata wafuasi wengi zaidi instagram kwa kufanya collabo

Baada ya hapa post content yako kama ni picha,video au reel kama kawaida unavyofanya siku zote. 

Post ikishachapishwa basi yule uliye collabo naye atapata ujumbe kwenye DM kuwa ametajwa kama mshiriki wa post na wewe.

Atapata mwito wa kukubali kama kweli mmekubaliana ku collabo, kama kila kitu kimekaa vizuri atakubali (accept). Au anaweza kukataa au kusitisha kwa muda ili mfanye mabadiliko ya kumridhisha zaidi.

Jinsi ya kupata wafuasi au followers zaidi Instaram

Akikubali (kwa kubonyeza accept) na wewe utapata ujumbe kuwa amekubali. Na baada ya hapo posti uliyochapisha itatokea na kwenye ukurasa wake yeye pia.

Hiyo ndio njia ya kwanza ya kupata wafuasi wengi zaidi kwa kufanya collab na akaunti nyingine za biashara.

#2: Karibisha wageni kwenye Instagram Live Room

Instagram Live Rooms ni kipengele cha huduma ya Instagram ambayo inakuruhusu kwenda live na watu hadi watatu kwa wakati mmoja.

Unachotakiwa kufanya ni kuchunguza watu gani wana maudhui ambayo yanaendanana biashara yako, kisha kuwasiliana nao na kuwaomba mfanye live session mkiongelea jambo ambalo litawafaidisha wote.

Kwa mfano wewe una duka la vifaa vya magari unaweza kwenda live na fundi magari na mkajadili mambo mbalimbali kuhusu changamoto za kumiliki magari na jinsi ya kuzitatua. 

Mtakapokuwa kwenye Live room wafuasi wenu wote watapata taarifa kuwa nyinyi wawili mnaingia live, kwa hiyo wote wakija kuwasikiliza wataweza kuwafahamu na kufahamiana.

Kwasababu mtakuwa mnawaelimisha bure kabisa, itakuwa rahisi sana kupata wafuasi wapya ambao wataweza kugeuka kuwa wateja wenu.

VITU VYA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA LIVE ROOM

  1. Watu sahihi wa kushirikisha: Fuata vigezo vya kuchagua mtu wa kufanya naye collabo ambavyo tumeshajadili hapo mwanzo. Ongeza kwa kuchagua mtu mchangamfu na anayeweza kujieleza vizuri ili watazamaji wafurahie.
  2. Muda: Mtakapopanga muda wa kwenda live basi hakikisha washiriki wote wanazingatia ili watazamaji wajue mpo professional. Msisahau pia kuzingatia muda wa kumaliza live.
  3. Ufahamu wa Live rooms: ikiwezekana mnaweza kufanya live za majaribio kabla ya live kuu ili kuhakikisha washiriki wote wanajua jinsi ya kujiunga kwenye live pale utakapowatumia mwaliko. Sio live imeshaanza na mmoja hajui hata kuingia au kuwasha mic asikike nk.
  4. Ubora wa internet: Hakikisha washiriki wote mna bundle la kutosha la kusapoti kuingia hewani kwa muda huo mliopanga. Hakuna kitu kibaya kama mtu kukatika katika au kutoweka kabisa kisa bundle kuisha au network kuwa mbaya. Watu huwa wanaacha kuangalia wakiona hivi.
  5. Ufasaha katika maogezi: wakati wa majadiliano hakikisheni mmoja anapoongea wengine wanakuwa kimya na kusikiliza badala ya kila mtu kuongea kwa wakati mmoja.
  6. Muongeaji mkuu: Ni vizuri zaidi yule ambaye akaunti yake imeanzisha live room awe ndiye moderator yaani kama mwongozaji wa maongezi. Yeye atakuwa anauliza maswali washiriki pia atakuwa na jukumu la kuongea na watazamaji ili kuhakikisha kuwa wanafuatilia live bila tatizo lolote. Muongeaji mkuu huwa anakuwa kama mtu kati ambaye anasoma maswali ya watazamaji na kuyawasilisha kwa wale washiriki aliowaalika.
  7. Muhtasari: Ni muhimu kwa muendeshaji mjadala au moderator kuwa anawapa summary au muhtasari wale watu wanaochelewa kuiangalia live. Hii itawasaidia na wao waweze kujiunga na maongezi badala ya kukata tamaa na kutoka offline pale wanapokuwa hawaelewi kitu.
  8. Save live video: Baada ya maongezi kuisha, aliyeanzisha live huwa anapewa chaguo la kuisave video nzima kwenye IGTV. Hii ni muhimu sana kwasababu watu waliokosa wataweza kuiangalia baadaye. Pia walioingia katikati wanaweza kurudi nyuma na kupitia walipokosa hivyo kufaidika kikamilifu.

Hii ni njia nzuri sana ya kupata wafuasi wengi zaidi kwa muda mfupi. Pata picha kama watu watatu mnaingia kwenye live na wote mna wafuasi labda 2,000 tu kila mmoja.

Hapa inamaana mna wafuasi 6,000 ambao mnaweza kubadilishana.

Na zaidi ya hapo, mnapotengeneza tabia ya kufanya live streams instagram itazidi kupromote akaunti zenu kwa watu wengine ili na wao waweze kufaidika na mnachosambaza.

SOMA: STIKA 10 ZINAZOONGEZA KOMENTI KWENYE INSTAGRAM

JINSI YA KUANZISHA INSTAGRAM LIVE ROOM

Ingia kwenye profile yako ya instagram yaani pale ambapo unaona picha zako zote na bio yako. Juu kulia utaona alama ya kujumlisha, Bonyeza kisha chagua LIVE, halafu weka kichwa cha habari cha live video.

Jinsi ya kupata wafuasi kwa kufanya Instagram Live

Ukiwa tayari kuanza kipindi cha live basi utabonyeza alama ya live. Mwanzoni kutakuwa hakuna watu au watakuwepo watu wachache.

Unaweza kutumia muda huu kuandaa vitu vyako na kuwasalimu waliowahi.

Unaweza kutumia nafasi hii pia kuwaambia watu wako kuhusu wageni watakaoingia kwenye live ya siku hiyo pamoja vitu ambavyo watategemea kujifunza.

Ukishaanzisha Live session basi wafuasi wako wote watapata ujumbe kuwa upo live na wataweza kujiunga.

Washiriki wakiwa tayari basi bonyeza picha ya camera ambayo utaiona kwenye screen. Hapo ukisearch jina la mtu unayetaka aingie live na ukalibonyeza jina lake, yeye atapata mwaliko wa kujiunga kwenye jopo la wachangiaji.

Akiukubali na yeye video yake itatokea live kwenye screen ya watu wote watakaokuwa wanaangalia wataweza kumuona na kumsikia.

Zaidi ya hayo, wafuasi wake watapata ujumbe kuwa mtu huyo ameingia kwenye live na wewe ,pia watapata mwaliko wa kujiunga kwa kuiangalia.

INSTAGRAM LIVE ROOM KWA AJILI YA KUPATA WATEJA

Kama ambavyo tumeshajadili hapo mwanzoni, hizi collaborations ni nzuri sana kwa ajili ya biashara kupata wafuasi wengi zaidi Instagram na kuongeza mauzo. 

Unaweza kualika mtu mwenye bidhaa zinazoendana na za kwako na mkaonesha jinsi ya kutumia bidhaa zenu kwa pamoja ili kupata muonekano au faida fulani.

Kwa kupitia maonesho hayo inakuwa rahisi zaidi kwa watu kununua bidhaa hizo kwa mkupuo kutoka kwenu kwasababu mnauza kwa njia nzuri sana ambayo ni ya maelekezo ya moja kwa moja.

Je umewahi kutumia mbinu hizi za jinsi kupata wafuasi wengi zaidi Instagram? 

Kama haujawahi kufanya Live rooms na Instagram collab feature usiendelee kubaki nyuma na kukosa faida kubwa katika mauzo pamoja na wafuasi.

KUMBUKA

Usikose kurudi Mjasiriamali Digital kila wiki kujifunza mbinu kabambe za kufanikiwa kibiashara katika jukwaa la Instagram. Pia karibu kwenye ukurasa wangu wa Instagram upate post mpya kila siku zenye dondoo za kugeuza wafuasi wako kuwa wateja wa kudumu.

Sasa ni wakati wa kuacha kubahatisha bahatisha instagram na kuanza kufanya bashara kiakili na kupata mafanikio zaidi!.

Share Makala Hii Kwa Wengine

Pata Kitabu

Hatua kwa hatua jinsi ya kuuza bidhaa online bila duka wala ofisi

Pata Kitabu

Pata copy yako leo uanze kutengeneza pesa kwenye Instagram

ZINAZOTREND