Wafanyabiashara wengi wanajua umuhimu wa kuposti mara kwa mara kwenye Instagram. Changamoto huja kwenye kujua wa posti nini ili kuepuka kurudia rudia picha. Katika makala hii nitakuonesha aina 13 za post nzuri kabisa kwa ajili ya akaunti ya instagram ya biashara
Aina 13 za post zinazoongeza wafuasi na mauzo kwa biashara Instagram
1: Posti za kuswipe(Carousels) zenye caption fupi
Jukwaa la Instagram limeundwa katika hali ambayo inafaa zaidi kuweka picha au video badala ya maneno mengi.
Watu wengi kweye jukwaa hili hupendelea kuona zaidi ya kusoma, ndio maana utakuta hata kama utoe maelekezo ya bidhaa na bei yake, bado kwenye comment utaona kuna watu wanaulizia bei na taarifa nyingine ambazo umeshaandika kwenye caption.
Kutokana na hili, badala ya kuweka Caption ndefu na picha moja, ni bora kuweka picha zenye maneno/ujumbe au maelekezo kisha kwenye caption uandike muhtasari tu na kuwaambia wa swipe kuona zaidi.
Wasiliana na mimi nikutengenezee picha nzuri za kuswipe (carousel) au nikufunze jinsi ya kutengeneza na kuweka maneno yenye muonekano mzuri na professional kwa ajili ya brand yako.
#2: Post za kuelimisha juu ya bidhaa au huduma
Ukweli ni kwamba wapo maelfu ya watu wanaouza bidhaa kupitia mitandao ya jamii kama Instagram. Kwanini mtu anunue bidhaa zako au alipie huduma zako badala ya za mwingine?
Moja ya njia madhubuti ya kuvutia wateja kwenye bidhaa zako ni kuwapa taarifa sahihi kuhusu bidhaa zako au huduma.
Wape watu moyo wa kununua kutoka kwako kwa kuwapa dondoo kuhusu unachofanya na kuhusu ubora wa bidhaa au huduma zako.
Kama unauza unga wa lishe basi weka post mbalimbali zinazochambua bidhaa hii ili mtu akiona iwe rahisi kwake kugundua ubora na kuamua kufanya manunuzi.
Hata kama una bidhaa nyingi sana, hakikisha unachambua moja moja katika post tofauti na uweke ratiba nzuri ya kuzirudia post hizi ila kwa kutumia picha tofauti na zile ambazo umeshawahi kupost.
#3: Posti za kuonesha jinsi ya kutumia bidhaa zako
Unapoposti hasa video zinazowaonesha watu jinsi bidhaa yako inavyoyafaidisha maisha yao basi una uhakika wa kuongeza wafuasi na wateja kutokana na sababu hizi tatu.
KWANZA: Unawasaidia wateja wako ambao tayari wamenunua kufahamu jinsi ya kutumia bidhaa. Hii itawafanya wapende kununua zaidi kutoka kwako kwasababu wanajua kuwa hawataweza kukwama kutumia bidhaa.
PILI: Utahamasisha wale watu ambao wanazijua bidhaa hizo sema tu walikuwa wanaghairi au kusita sita kuzinunua. Wakiona video ya uzuri wa bidhaa na urahisi wa kuzitumia basi mara nyingi watapata munkari wa kununua mara moja!.
TATU: Utafanya hata watu ambao hawakujua kuwa wanahitaji bidhaa kama hiyo kwenye maisha yao waweze kununua kutoka kwako. Hii huwa ni kwasababu tu ya kuvutiwa papo hapo na lile onesho la jinsi bidhaa inavyofanya kazi.
INSTAGRAM LIVE ZA MAUZO
Unaweza kutumia Instagram Live kama njia ya kuwaonesha wafuasi wako jinsi ya kutumia bidhaa zako. Hii itawahakikishia pia kuwa hakuna ugumu kwasababu umeonesha hatua zote ukiwa live bila kuedit.
Ukiuliza wafanyabiashara wengi wanaouza bidhaa nyingi sana kupitia Instagram watakuambia kuwa video za aina hii zina faida sana.
Unaweza kuzipost kama video za IGTV, Instagram story au bora kuliko zote unaweza kuzifupisha na kuwa INSTAGRAM REELS!.
Kama wewe ni mfuasi wa Mjasiriamali Digital basi utakuwa tayari unafahamu kuwa Instagram reels ndio kwenye views nyingi zaidi hivyo uwezekano mkubwa zaidi kufikia wateja wengi zaidi kuliko picha au video tu za IGTV.
#4: Post za before and after
Je, una bidhaa au huduma ambazo hubadilisha muonekano wa kitu au mtu na kuuboresha?
Kama jibu lako ni ndio basi katika hizi aina 13 za post tunazoenda kujadili, hii itakuwa na faida kwako kuliko nyingine zote!
Badala ya kuongelea tu kuhusu ubora wa bidhaa ni bora kujikita katika kupiga picha za kabla huduma au bidhaa haijatumika na kupiga baada ya utumiaji.
Aina hii ya post ina faida sana kwa bidhaa au huduma za kupunguza/kuongeza uzito, Saloon za kiume na za kike, huduma za makeup, mafundi wa aina nyingi hasa wanaotengeneza au kurepair vitu, wauzaji wa wallpapers na urembo aina nyingine wa nyumbani nk
Post hizi huwa nzuri zaidi zikiwa kwenye Carousel yaani zile za ku-swipe badala ya kuwa tu picha moja yenye before and after.
Mara nyingi inashauriwa kuanza na picha ya before na kuaambia watu wa swipe kuona ya after na kisha picha ya mwisho ndio iwe ile moja yenye zote mbili.
Au unaweza kuanza na after na uwaelekeze wa-swipe ili kuona hali ilivyokuwa mwanzoni kisha kumalizia na ile picha moja yenye zote mbili.
#5: Posti bidhaa mpya.
Watangazie wafuasi na wateja kuhusu bidhaa au huduma mpya zinazopatikana katika biashara yako. Piga picha mbali mbali ili uweze kupost nyingi kwa wakati mmoja na wao waweze kuswipe na kuona muonekano tofauto au rangi tofauti za bishaa hizo mpya.
#6: StyleBidhaa yako na bidhaa nyingine.
Bidhaa kama nguo, fenicha , make up, vifaa vya nyumbani, urembo, huvutia zaidi pale zinapooneshwa jinsi zinavyoendana na vitu vingine.
Kwa mfano mtu anayeuza nguo kama magauni, anaweza kuposti picha za magauni anayouza yakiwa yamevaliwa na vitu vingine kama viatu, pochi, saa, kofia nk.
Muuza coffe table anaweza kuweka picha za meza zake zikiwa kwenye mazulia tofauti, kwenye sebule zenye masofa tofauti au zikiwa na vyungu vya maua tofauti. Pia zikiwa sehemu tofauti kama sebuleni, kwenye Balcony, chumbani nk.
Kama tayari na hizi bidhaa nyingine unazo basi ni rahisi kwa kupata mauzo zaidi kwasababu mtu anapopenda ile package ya muonekano hupendelea zaidi kuokoa muda wa kutafuta kitu kimoja kimoja na kuamua kununua vyote kwa mkupuo.
Lakini kama hauna hizo bidhaa nyingine si mbaya pia kwasababu kuuza utakuwa umeuza. Pia utakuwa umemsaidia mteja wako kupata wazo zuri la jinsi ya kwenda kustyle bidhaa hiyo na vitu vingine.
Lakini bora zaidi unaweza kufanya collabo na mfanyabiashara mwingine mwenye hizo bidhaa nyingine ili wateja wako wapate kuokoa muda na kununua kwenu.
Ukimaliza kuzipitia hizi aina 13 za post zenye manufaa kwa akaunti ya biashara yako usikose kupitia makala ifuatayo ili kuhakikisha unapata dondoo zaidi kwa ajili ya mafanikio makubwa zaidi.
Ili kupata wateja wengi zaidi kwaajili ya bidhaa fulani ni muhimu sana kuanza kuongelea bidhaa hizo kabla hata haujaanza kuziuza.
Nenda online na utafute picha nzuri za bidhaa kisha uwaoneshe wafuasi wako kuwa zinaanza kuuzwa tarehe fulani.
Ikiwezekana waambie wale wanaohitaji wakuruhusu uwakumbushe inbox siku ile ambayo bidhaa inafika dukani ili zisije kuisha kabla hawajapata.
Kama bidhaa zako zinatoka nje ya nchi basi hakikisha tarehe ya mzigo kuwasili kabla haujaitangaza.
Kama utatangaza tarehe na huku mzigo ukachelewa basi itakuwa kero kwa wafuasi wako ambao tayari walikuwa wanasubiria tarehe ile kwa hamu.
Ni bora kuacha siku chache au hata wiki moja kati ya siku mzigo wako unapotegemewa kufika kwako hadi siku ambayo umetangaza kuanza kupatikana kwa bidhaa hizo.
#8: Post za behind the scenes
Hizi ni zile posti ambazo zinaonesha jinsi biashara yako inavyoendeshwa au jinsi bidhaa zinavyotengenezwa.
Kwa mfano unatoa huduma za makeup, unnaweza kuonesha vipengele vifupi tu vya jinsi unavyotoa huduma hii kwa wateja wako.
Mafundi wa masofa wanaweza kuonesha ofisi zao na kiasi kidogo tu cha jinsi wanavyotengeneza bidhaa zao nzuri.
Waandaaji wa keki za shughuli wanaweza kuonesha jinsi wanavyochanganya mahitaji hadi keki zinapokamilika nk.
Si lazima uoneshe kila kitu bali vipande vifupi vifupi tu ili watu wapate picha kidogo ya jinsi biashara yako inavyoenda.
Unaweza pia kuonesha unavyo-deliver mizigo kwa wateja wako. Kama biashara yako ni ya huduma kama hoteli unaweza kuonesha video za jinsi wasafishaji wanavyoandaa vyumba au jinsi wapishi wanavyoandaa vyakula jikoni.
Au pia unaweza tu kupost picha/video zinazoonesha jinsi unavyofanya kazi ofisini kwako.
Faida ya posti kama hizi ni kwamba zinaonesha wafuasi wako pamoja na watu wapya wasiofahamu biashara yako kuwa wewe sio tapeli, unafanya kazi vizuri, unatoa huduma vizuri na unafurahia kazi yako.
Inakuonesha kuwa wewe ni mtu wa ukweli na sio mtu asiyejulikana ambaye huwa anaposti tu na kuandika captions.
Kwa kifupi katika enzi hii ambapo matapeli mitandaoni wapo, post za behind the scenes zinajenga imani zaidi kati ya wafuasi/wateja na wauzaji/watoa huduma.
#9: Promote tukio maalumu
Kama vile kampuni au biashara yako inaadhimia kuendesha tukio la muhimu kama vile conference, tamasha, darasa, sherehe,safari, harambee au mengineyo unaweza kutengeneza post za aina mbalimbali ili kutangaza tukio hilo.
Baadhi ya post unazoweza kuweka ni kama zifuatazo:
Lengo la tukio, muda na mahali litakapotokea
Post kuhusu mambo yatakayojiri ili kuwapa watu motisha ya kuhudhuria.
Post za ofa ya punguzo la bei kwa kundi fulani la watu mfano watoto au wanawake au kwa wale watakaonunua tiketi mapema.
#10: Post za maswali
Ili ukurasa wako na post zako zifikie watu wengi zaidi inatakiwa mitambo ya Instagram igundue kuwa watu wanafurahia na kufaidika na posti zako au za biashara yako.
Njia inayotumika kugundua kuwa watu wanafurahia vitu unavyopost ni kupitia LIKES,KOMENTI, SAVES na SHARES unazopata.
Kiutaalamu hii inaitwa engagement, yaani ni kipimo cha jinsi watu wanavyoonesha ushirikiano na posti zako.
Moja ya njia bora zaidi ya kupata komenti nyingi kwenye Instagram ni kupitia maswali.
Unapoweka posti yenye swali linalohamasisha kujibiwa basi utakuwa unapata komenti nyingi na kufanya instagram ioneshe posti zako kwa watu wengi zaidi wapya hivyo kukuongezea nafasi ya kupata wafuasi na wateja zaidi.
Faida nyingine ya maswali ni kwamba utaweza kufahamu vitu ambavyo wafuasi wako wanapenda hivyo kukupa mawazo ya bidhaa zitakazouzika zaidi.
Kwa mfano kama duka lako linauza nguo aina ya jeans unaweza kuuliza swali kama:
Kwenye kabati lako kuna jeans aina zipi nyingi zaidi?
A. Nyeusi
B. Blue
C. Blue bahari (mpauko)
D. Sipendelei kuvaa Jeans
Hii itakusaidia kujua walengwa wako wanapendelea rangi zipi hivyo uziongeze na kuepuka zisizopendelewa.
Au badala ya maswali unaweza kutuma posti ambazo zinawaambia wafuasi wako wafanye kitu fulani mfano waite marafiki zao kwa kuwatag kwenye komenti.
Kwa mfano unaweza kuweka picha ya Pizza inayopendwa kwenye restaurant yako kisha kwenye caption ukasema kitu kama “Tag mtu yoyote ambaye anaweza kumaliza pizza hii peke yake”
Wasiliana na mimi nikuelekeze kiundani jinsi ya kuunda maswali yanayoendana na biashara yako na yenye kufanya watu wahamasike kujibu.
#11: Karibisha wafuasi/wateja wapost kuhusu biashara yako
Moja ya njia bora ya kuhamasisha watu kuamini huduma/bidhaa zako ni kuwaonesha kuwa watu wengine wanazitumia na kuzifurahia ni kupitia njia hii.
Ili kufanikisha hili, tuma posti za kuomba mrejesho na pia omba wateja wako wapost au wakutumie DM picha zao wakiwa na bidhaa zako au wakipata huduma kwenye eneo lako la biashara.
Wanapoposti kwenye kurasa zao na kukutag au kutag kampuni/biashara, usipoteze nafasi hii ya kurepost kwenye kurasa yako pia.
Hii itasaidia kwanza yule mfuasi aliyepost ajisikie furaha kwamba umetambua posti yake na umeifurahia.
Lakini pia itakupatia wafuasi zaidi kwasababu watatambua kuwa huduma ni nzuri hadi watu wanaposti. Pia biashara/kampuni ni nzuri hadi inachukua muda kuwapost wateja wake kwenye kurasa yao.
#12: Posti za mashindano au za kugawa zawadi(Giveaways)
Njia nyingine nzuri ya kuongeza ushirikiano kati ya watu na posti za biashara yako (yaani kuongeza engagement) ni kufanya mashindano kwenye ukurasa wako.
Katika upande wa mashindano unachotakiwa kufanya ni kuwaambia watu wafanye vitu vifuatavyo ili kuweza kujipatia nafasi ya kushinda:
WAKUFOLLOW: Mshindi anatakiwa kuwa mfuasi wa biashara au kampuni yako. Kwa hiyo katika posti ya tangazo lazima uwaambie washiriki kuwa wakitaka kuingia kwenye mchuano ni lazima wahakikishe kuwa tayari ni wafuasi.
LIKE: Hii ni mbinu ya kwanza na rahisi ya kuongeza engagement kwenye posti yako. Mtu yeyote anayeamua kushiriki kwenye shindano ni lazima atakuwa amependa jambo hili. Kwa hiyo ni kitu rahisi kuwakumbusha ku like posti mapema kabla ya mengine.
KOMENTI: Ili kuongeza engagement na kusaidia instagram ipeleke posti hii kwenye macho ya watu wengi zaidi, waambie watu wanaotaka kuingia kwenye shindano au wanaotaka kuingia kwenye droo ya kupata zawadi waandike ujumbe fulani kwenye komenti. Ujumbe unaweza kuwa wowote ule lakini ni vizuri kama utaendana na maudhui ya biashara yako. Kwa mfano kama wewe unauza mashine za kusagia juisi au blenders unaweza kuwaambia kuwa kama mtu anataka kuingizwa kwenye shindano basi aandike kwenye komenti aina ya juisi anayoipenda zaidi. Hii pia itakusaidia wewe kuweza kugundua kupitia komenti kuwa ni wafuasi wepi wanatakiwa majina yao yaingizwe kwenye mchuano.
TAG WATU WENGINE: Waambie washiriki wawa-tag au watu wao wa karibu ambao wanaweza kuvutiwa na biashara au huduma yako.
Ku-tag ni njia ya kufanya mtu mwingine mwenye akaunti ya instagram aweze kufika kwenye posti fulani kwa kuandika alama hii @ pamoja na jina lake analotumia instagram.
Kwa hiyo mfuasi anapoona shindano na kutag watu wake na wao wanapata nafasi ya kuona posti yako ya tangazo na kuhamasika na wao kujiunga na shindano.
Hii inamaanisha utapata wafuasi wengi wapya kutoka kwa wafuasi ambao unao. Wafuasi hawa wapya nao ili kushinda wata-tag wenzao wengine.
Kwa hiyo mwisho wa tangazo unajikuta na wafuasi wengi zaidi kuliko kama ungeposti tu posti ya kawaida ambayo sio ya shindano.
#13: Post ya vichekesho au Meme
Waoneshe wafuasi wako kuwa wewe au kampuni/biashara yako ni wa kihalisia kwa kuwafurahisha hapa na pale kwa kutumia vichekesho vya memes.
Post za memes huwa ni nzuri kwasababu watu huzi-LIKE zaidi na pia ni rahisi kwa wao kuzi-share na watu wao wa karibu kwa kuwatumia au kuwa-tag.
Ukichagua memes ambazo zinaendana na maudhui ya biashara/kampuni yako utakuwa na uhakika mkubwa zaidi kuwa wafuasi wako na watu wapya wanaofurahia maudhui haya wataguswa na kuchekeshwa.
Hii husaidia sana katika kufanya brand yako ipendwe na watu wengi zaidi. Haitakiwi kila siku utume posti za biashara tuu au za kuwa serious tu.
Ukipost na viburudisho kidogo itawaonesha wafuasi wako kuwa wewe haujali tu kutengeneza pesa kupitia wao bali unapenda pia wafurahi na wacheke pamoja na wewe.
Kwa kifupi:
Hizi aina 13 za post zina manufaa makubwa sana kwa kurasa za biashara Instagram kwasababu zinafanya watu wa like, share na kukomenti zaidi kwenye posti.
Hali hii hupelekea instagram wagundue kuwa kurasa ya kampuni/biashara yako inapendwa sana hivyo kuionesha kwa watu wengi zaidi huku ikikufanya wewe kupata wafuasi wengi zaidi.
Kumbuka sio kwamba ni lazima kupost zote aina 13 za post nilizozitaja katika makala hii. Unaweza kuchagua baadhi ambazo unazimudu na ukawa unachapisha hizo tu,
Lakini kwasababu wafanyabiashara wanatakiwa kuposti mara kwa mara, ni bora kujaribu aina nyingi ili kukuepusha kukaa muda mrefu bila kuposti.
Wasiliana na mimi ili nikutengenezee au nikufundishe jinsi ya kutengeneza posti nzuri za mwezi za aina hii ili kunufaisha biashara yako kwa kiasi kikubwa zaidi ya ilipo sasa.
Katika sehemu ya komenti niambie ni aina ipi kati ya hizi aina13 za posti umekuwa ukitumia na zikakuletea manufaa zaidi?.
Endelea kufuatilia Mjasiriamali Digital kupata dondoo makini sana za kuongeza wafuasi na mauzo kwa ajili ya biashara yako katika jukwaa la instagram.
Share Makala Hii Kwa Wengine
Pata Kitabu
Hatua kwa hatua jinsi ya kuuza bidhaa online bila duka wala ofisi
Pata Kitabu
Pata copy yako leo uanze kutengeneza pesa kwenye Instagram
Aina 13 za post za Instagram kwa akaunti za biashara
Table of Contents
Wafanyabiashara wengi wanajua umuhimu wa kuposti mara kwa mara kwenye Instagram. Changamoto huja kwenye kujua wa posti nini ili kuepuka kurudia rudia picha. Katika makala hii nitakuonesha aina 13 za post nzuri kabisa kwa ajili ya akaunti ya instagram ya biashara
Aina 13 za post zinazoongeza wafuasi na mauzo kwa biashara Instagram
1: Posti za kuswipe(Carousels) zenye caption fupi
Jukwaa la Instagram limeundwa katika hali ambayo inafaa zaidi kuweka picha au video badala ya maneno mengi.
Watu wengi kweye jukwaa hili hupendelea kuona zaidi ya kusoma, ndio maana utakuta hata kama utoe maelekezo ya bidhaa na bei yake, bado kwenye comment utaona kuna watu wanaulizia bei na taarifa nyingine ambazo umeshaandika kwenye caption.
Kutokana na hili, badala ya kuweka Caption ndefu na picha moja, ni bora kuweka picha zenye maneno/ujumbe au maelekezo kisha kwenye caption uandike muhtasari tu na kuwaambia wa swipe kuona zaidi.
Wasiliana na mimi nikutengenezee picha nzuri za kuswipe (carousel) au nikufunze jinsi ya kutengeneza na kuweka maneno yenye muonekano mzuri na professional kwa ajili ya brand yako.
#2: Post za kuelimisha juu ya bidhaa au huduma
Ukweli ni kwamba wapo maelfu ya watu wanaouza bidhaa kupitia mitandao ya jamii kama Instagram. Kwanini mtu anunue bidhaa zako au alipie huduma zako badala ya za mwingine?
Moja ya njia madhubuti ya kuvutia wateja kwenye bidhaa zako ni kuwapa taarifa sahihi kuhusu bidhaa zako au huduma.
Wape watu moyo wa kununua kutoka kwako kwa kuwapa dondoo kuhusu unachofanya na kuhusu ubora wa bidhaa au huduma zako.
Kama unauza unga wa lishe basi weka post mbalimbali zinazochambua bidhaa hii ili mtu akiona iwe rahisi kwake kugundua ubora na kuamua kufanya manunuzi.
Hata kama una bidhaa nyingi sana, hakikisha unachambua moja moja katika post tofauti na uweke ratiba nzuri ya kuzirudia post hizi ila kwa kutumia picha tofauti na zile ambazo umeshawahi kupost.
#3: Posti za kuonesha jinsi ya kutumia bidhaa zako
Unapoposti hasa video zinazowaonesha watu jinsi bidhaa yako inavyoyafaidisha maisha yao basi una uhakika wa kuongeza wafuasi na wateja kutokana na sababu hizi tatu.
KWANZA: Unawasaidia wateja wako ambao tayari wamenunua kufahamu jinsi ya kutumia bidhaa. Hii itawafanya wapende kununua zaidi kutoka kwako kwasababu wanajua kuwa hawataweza kukwama kutumia bidhaa.
PILI: Utahamasisha wale watu ambao wanazijua bidhaa hizo sema tu walikuwa wanaghairi au kusita sita kuzinunua. Wakiona video ya uzuri wa bidhaa na urahisi wa kuzitumia basi mara nyingi watapata munkari wa kununua mara moja!.
TATU: Utafanya hata watu ambao hawakujua kuwa wanahitaji bidhaa kama hiyo kwenye maisha yao waweze kununua kutoka kwako. Hii huwa ni kwasababu tu ya kuvutiwa papo hapo na lile onesho la jinsi bidhaa inavyofanya kazi.
INSTAGRAM LIVE ZA MAUZO
Unaweza kutumia Instagram Live kama njia ya kuwaonesha wafuasi wako jinsi ya kutumia bidhaa zako. Hii itawahakikishia pia kuwa hakuna ugumu kwasababu umeonesha hatua zote ukiwa live bila kuedit.
Ukiuliza wafanyabiashara wengi wanaouza bidhaa nyingi sana kupitia Instagram watakuambia kuwa video za aina hii zina faida sana.
Unaweza kuzipost kama video za IGTV, Instagram story au bora kuliko zote unaweza kuzifupisha na kuwa INSTAGRAM REELS!.
Kama wewe ni mfuasi wa Mjasiriamali Digital basi utakuwa tayari unafahamu kuwa Instagram reels ndio kwenye views nyingi zaidi hivyo uwezekano mkubwa zaidi kufikia wateja wengi zaidi kuliko picha au video tu za IGTV.
#4: Post za before and after
Je, una bidhaa au huduma ambazo hubadilisha muonekano wa kitu au mtu na kuuboresha?
Kama jibu lako ni ndio basi katika hizi aina 13 za post tunazoenda kujadili, hii itakuwa na faida kwako kuliko nyingine zote!
Badala ya kuongelea tu kuhusu ubora wa bidhaa ni bora kujikita katika kupiga picha za kabla huduma au bidhaa haijatumika na kupiga baada ya utumiaji.
Aina hii ya post ina faida sana kwa bidhaa au huduma za kupunguza/kuongeza uzito, Saloon za kiume na za kike, huduma za makeup, mafundi wa aina nyingi hasa wanaotengeneza au kurepair vitu, wauzaji wa wallpapers na urembo aina nyingine wa nyumbani nk
Post hizi huwa nzuri zaidi zikiwa kwenye Carousel yaani zile za ku-swipe badala ya kuwa tu picha moja yenye before and after.
Mara nyingi inashauriwa kuanza na picha ya before na kuaambia watu wa swipe kuona ya after na kisha picha ya mwisho ndio iwe ile moja yenye zote mbili.
Au unaweza kuanza na after na uwaelekeze wa-swipe ili kuona hali ilivyokuwa mwanzoni kisha kumalizia na ile picha moja yenye zote mbili.
#5: Posti bidhaa mpya.
Watangazie wafuasi na wateja kuhusu bidhaa au huduma mpya zinazopatikana katika biashara yako. Piga picha mbali mbali ili uweze kupost nyingi kwa wakati mmoja na wao waweze kuswipe na kuona muonekano tofauto au rangi tofauti za bishaa hizo mpya.
#6: Style Bidhaa yako na bidhaa nyingine.
Bidhaa kama nguo, fenicha , make up, vifaa vya nyumbani, urembo, huvutia zaidi pale zinapooneshwa jinsi zinavyoendana na vitu vingine.
Kwa mfano mtu anayeuza nguo kama magauni, anaweza kuposti picha za magauni anayouza yakiwa yamevaliwa na vitu vingine kama viatu, pochi, saa, kofia nk.
Muuza coffe table anaweza kuweka picha za meza zake zikiwa kwenye mazulia tofauti, kwenye sebule zenye masofa tofauti au zikiwa na vyungu vya maua tofauti. Pia zikiwa sehemu tofauti kama sebuleni, kwenye Balcony, chumbani nk.
Kama tayari na hizi bidhaa nyingine unazo basi ni rahisi kwa kupata mauzo zaidi kwasababu mtu anapopenda ile package ya muonekano hupendelea zaidi kuokoa muda wa kutafuta kitu kimoja kimoja na kuamua kununua vyote kwa mkupuo.
Lakini kama hauna hizo bidhaa nyingine si mbaya pia kwasababu kuuza utakuwa umeuza. Pia utakuwa umemsaidia mteja wako kupata wazo zuri la jinsi ya kwenda kustyle bidhaa hiyo na vitu vingine.
Lakini bora zaidi unaweza kufanya collabo na mfanyabiashara mwingine mwenye hizo bidhaa nyingine ili wateja wako wapate kuokoa muda na kununua kwenu.
Ukimaliza kuzipitia hizi aina 13 za post zenye manufaa kwa akaunti ya biashara yako usikose kupitia makala ifuatayo ili kuhakikisha unapata dondoo zaidi kwa ajili ya mafanikio makubwa zaidi.
SOMA: JINSI YA KUPATA WAFUASI NA MAUZO ZAIDI KWA KUFANYA COLLABO NA WAFANYABIASHARA WENGINE.
#7: Post bidhaa ambazo bado hazijaanza kuuzwa.
Ili kupata wateja wengi zaidi kwaajili ya bidhaa fulani ni muhimu sana kuanza kuongelea bidhaa hizo kabla hata haujaanza kuziuza.
Nenda online na utafute picha nzuri za bidhaa kisha uwaoneshe wafuasi wako kuwa zinaanza kuuzwa tarehe fulani.
Ikiwezekana waambie wale wanaohitaji wakuruhusu uwakumbushe inbox siku ile ambayo bidhaa inafika dukani ili zisije kuisha kabla hawajapata.
Kama bidhaa zako zinatoka nje ya nchi basi hakikisha tarehe ya mzigo kuwasili kabla haujaitangaza.
Kama utatangaza tarehe na huku mzigo ukachelewa basi itakuwa kero kwa wafuasi wako ambao tayari walikuwa wanasubiria tarehe ile kwa hamu.
Ni bora kuacha siku chache au hata wiki moja kati ya siku mzigo wako unapotegemewa kufika kwako hadi siku ambayo umetangaza kuanza kupatikana kwa bidhaa hizo.
#8: Post za behind the scenes
Hizi ni zile posti ambazo zinaonesha jinsi biashara yako inavyoendeshwa au jinsi bidhaa zinavyotengenezwa.
Kwa mfano unatoa huduma za makeup, unnaweza kuonesha vipengele vifupi tu vya jinsi unavyotoa huduma hii kwa wateja wako.
Mafundi wa masofa wanaweza kuonesha ofisi zao na kiasi kidogo tu cha jinsi wanavyotengeneza bidhaa zao nzuri.
Waandaaji wa keki za shughuli wanaweza kuonesha jinsi wanavyochanganya mahitaji hadi keki zinapokamilika nk.
Si lazima uoneshe kila kitu bali vipande vifupi vifupi tu ili watu wapate picha kidogo ya jinsi biashara yako inavyoenda.
Unaweza pia kuonesha unavyo-deliver mizigo kwa wateja wako. Kama biashara yako ni ya huduma kama hoteli unaweza kuonesha video za jinsi wasafishaji wanavyoandaa vyumba au jinsi wapishi wanavyoandaa vyakula jikoni.
Au pia unaweza tu kupost picha/video zinazoonesha jinsi unavyofanya kazi ofisini kwako.
Faida ya posti kama hizi ni kwamba zinaonesha wafuasi wako pamoja na watu wapya wasiofahamu biashara yako kuwa wewe sio tapeli, unafanya kazi vizuri, unatoa huduma vizuri na unafurahia kazi yako.
Inakuonesha kuwa wewe ni mtu wa ukweli na sio mtu asiyejulikana ambaye huwa anaposti tu na kuandika captions.
Kwa kifupi katika enzi hii ambapo matapeli mitandaoni wapo, post za behind the scenes zinajenga imani zaidi kati ya wafuasi/wateja na wauzaji/watoa huduma.
#9: Promote tukio maalumu
Kama vile kampuni au biashara yako inaadhimia kuendesha tukio la muhimu kama vile conference, tamasha, darasa, sherehe,safari, harambee au mengineyo unaweza kutengeneza post za aina mbalimbali ili kutangaza tukio hilo.
Baadhi ya post unazoweza kuweka ni kama zifuatazo:
#10: Post za maswali
Ili ukurasa wako na post zako zifikie watu wengi zaidi inatakiwa mitambo ya Instagram igundue kuwa watu wanafurahia na kufaidika na posti zako au za biashara yako.
Njia inayotumika kugundua kuwa watu wanafurahia vitu unavyopost ni kupitia LIKES,KOMENTI, SAVES na SHARES unazopata.
Kiutaalamu hii inaitwa engagement, yaani ni kipimo cha jinsi watu wanavyoonesha ushirikiano na posti zako.
Moja ya njia bora zaidi ya kupata komenti nyingi kwenye Instagram ni kupitia maswali.
Unapoweka posti yenye swali linalohamasisha kujibiwa basi utakuwa unapata komenti nyingi na kufanya instagram ioneshe posti zako kwa watu wengi zaidi wapya hivyo kukuongezea nafasi ya kupata wafuasi na wateja zaidi.
Faida nyingine ya maswali ni kwamba utaweza kufahamu vitu ambavyo wafuasi wako wanapenda hivyo kukupa mawazo ya bidhaa zitakazouzika zaidi.
Kwa mfano kama duka lako linauza nguo aina ya jeans unaweza kuuliza swali kama:
Kwenye kabati lako kuna jeans aina zipi nyingi zaidi?
A. Nyeusi
B. Blue
C. Blue bahari (mpauko)
D. Sipendelei kuvaa Jeans
Hii itakusaidia kujua walengwa wako wanapendelea rangi zipi hivyo uziongeze na kuepuka zisizopendelewa.
Au badala ya maswali unaweza kutuma posti ambazo zinawaambia wafuasi wako wafanye kitu fulani mfano waite marafiki zao kwa kuwatag kwenye komenti.
Kwa mfano unaweza kuweka picha ya Pizza inayopendwa kwenye restaurant yako kisha kwenye caption ukasema kitu kama “Tag mtu yoyote ambaye anaweza kumaliza pizza hii peke yake”
Wasiliana na mimi nikuelekeze kiundani jinsi ya kuunda maswali yanayoendana na biashara yako na yenye kufanya watu wahamasike kujibu.
#11: Karibisha wafuasi/wateja wapost kuhusu biashara yako
Moja ya njia bora ya kuhamasisha watu kuamini huduma/bidhaa zako ni kuwaonesha kuwa watu wengine wanazitumia na kuzifurahia ni kupitia njia hii.
Ili kufanikisha hili, tuma posti za kuomba mrejesho na pia omba wateja wako wapost au wakutumie DM picha zao wakiwa na bidhaa zako au wakipata huduma kwenye eneo lako la biashara.
Wanapoposti kwenye kurasa zao na kukutag au kutag kampuni/biashara, usipoteze nafasi hii ya kurepost kwenye kurasa yako pia.
Hii itasaidia kwanza yule mfuasi aliyepost ajisikie furaha kwamba umetambua posti yake na umeifurahia.
Lakini pia itakupatia wafuasi zaidi kwasababu watatambua kuwa huduma ni nzuri hadi watu wanaposti. Pia biashara/kampuni ni nzuri hadi inachukua muda kuwapost wateja wake kwenye kurasa yao.
#12: Posti za mashindano au za kugawa zawadi(Giveaways)
Njia nyingine nzuri ya kuongeza ushirikiano kati ya watu na posti za biashara yako (yaani kuongeza engagement) ni kufanya mashindano kwenye ukurasa wako.
Katika upande wa mashindano unachotakiwa kufanya ni kuwaambia watu wafanye vitu vifuatavyo ili kuweza kujipatia nafasi ya kushinda:
Ku-tag ni njia ya kufanya mtu mwingine mwenye akaunti ya instagram aweze kufika kwenye posti fulani kwa kuandika alama hii @ pamoja na jina lake analotumia instagram.
Kwa hiyo mfuasi anapoona shindano na kutag watu wake na wao wanapata nafasi ya kuona posti yako ya tangazo na kuhamasika na wao kujiunga na shindano.
Hii inamaanisha utapata wafuasi wengi wapya kutoka kwa wafuasi ambao unao. Wafuasi hawa wapya nao ili kushinda wata-tag wenzao wengine.
Kwa hiyo mwisho wa tangazo unajikuta na wafuasi wengi zaidi kuliko kama ungeposti tu posti ya kawaida ambayo sio ya shindano.
#13: Post ya vichekesho au Meme
Waoneshe wafuasi wako kuwa wewe au kampuni/biashara yako ni wa kihalisia kwa kuwafurahisha hapa na pale kwa kutumia vichekesho vya memes.
Post za memes huwa ni nzuri kwasababu watu huzi-LIKE zaidi na pia ni rahisi kwa wao kuzi-share na watu wao wa karibu kwa kuwatumia au kuwa-tag.
Ukichagua memes ambazo zinaendana na maudhui ya biashara/kampuni yako utakuwa na uhakika mkubwa zaidi kuwa wafuasi wako na watu wapya wanaofurahia maudhui haya wataguswa na kuchekeshwa.
Hii husaidia sana katika kufanya brand yako ipendwe na watu wengi zaidi. Haitakiwi kila siku utume posti za biashara tuu au za kuwa serious tu.
Ukipost na viburudisho kidogo itawaonesha wafuasi wako kuwa wewe haujali tu kutengeneza pesa kupitia wao bali unapenda pia wafurahi na wacheke pamoja na wewe.
Kwa kifupi:
Hizi aina 13 za post zina manufaa makubwa sana kwa kurasa za biashara Instagram kwasababu zinafanya watu wa like, share na kukomenti zaidi kwenye posti.
Hali hii hupelekea instagram wagundue kuwa kurasa ya kampuni/biashara yako inapendwa sana hivyo kuionesha kwa watu wengi zaidi huku ikikufanya wewe kupata wafuasi wengi zaidi.
Kumbuka sio kwamba ni lazima kupost zote aina 13 za post nilizozitaja katika makala hii. Unaweza kuchagua baadhi ambazo unazimudu na ukawa unachapisha hizo tu,
Lakini kwasababu wafanyabiashara wanatakiwa kuposti mara kwa mara, ni bora kujaribu aina nyingi ili kukuepusha kukaa muda mrefu bila kuposti.
Wasiliana na mimi ili nikutengenezee au nikufundishe jinsi ya kutengeneza posti nzuri za mwezi za aina hii ili kunufaisha biashara yako kwa kiasi kikubwa zaidi ya ilipo sasa.
Katika sehemu ya komenti niambie ni aina ipi kati ya hizi aina13 za posti umekuwa ukitumia na zikakuletea manufaa zaidi?.
Endelea kufuatilia Mjasiriamali Digital kupata dondoo makini sana za kuongeza wafuasi na mauzo kwa ajili ya biashara yako katika jukwaa la instagram.
Share Makala Hii Kwa Wengine
Pata Kitabu
Hatua kwa hatua jinsi ya kuuza bidhaa online bila duka wala ofisi
Pata Kitabu
Pata copy yako leo uanze kutengeneza pesa kwenye Instagram
ZINAZOTREND
Sababu 3 kwanini utumie facebook ads 2022
Sababu 6 kwanini haupati wafuasi wa maana