Hivi ilishawahi kukutokea siku uliamua kuangalia wafuasi wako kwenye akaunti ya biashara ya Instagram na kuona kadiri siku zinavyoenda na wafuasi wako wanapungua kwenye akaunti yako. Baada ya wiki unashangaa unapoteza wafuasi 20, 100 au zaidi unajisikiaje? Vizuri kwa kujibu unajisikia vibaya si ndio?
Kuanzia leo nataka usijisikie vibaya na uanze kujisikia vizuri kwa kuona kuna watu (Wafuasi wako) wanataka kujifunza kutoka kwako, na kila siku watu wana unfollow na kupoteza wafuasi 100, 50,100, 1,000 au zaidi
Naomba nikulize swali moja…
Je, unaweza kufanya watu wasiku-unfollow kwenye akaunti yako ya biashara ya Instagram? Unagundua huwezi kufanya wasiku-unfollow bali ni kuwapa sababu za kufanya waendelee kubaki katika akaunti yako na hata kupata wafuasi wapya.
Leo utayajua Mambo 6 ya kufanya ili usiwapoteze wafuasi katika akaunti yako ya instagram, si upo tayari? Basi twende kupata madini ya nguvu;
#1 Angalia performance ya machapisho yako kwenye Insights
Akaunti yako ya Business au ya Creator unaweza kuangalia machapisho gani yanafanya vizuri katika akaunti yako, ni post gani ambazo zina share nyingi, ni post gani imepata likes nyingi, ni post gani imepata comment gani, ni post gani imepata save nyingi.
Kuangalia aina gani ya maudhui yaani Content zimepata kuungana na wafuasi wako kwa maana ya “Interaction” ya kutosha na anza kutumia idea ile ile au unaweza kuongeza ubunifu na utofauti kidogo lakini inakuwa inazungumzia topic ile ile; wewe unachofanya ni ni kurudia kwa namna fulani ambayo inazungumzia mada husika.
Angalia Insight kwenye akaunti yako kujua ni aina gani ya machapisho yanayofanya vizuri, kisha wewe unakuwa unarudia kwa mpangilio, lakini unaongeza ubunifu na kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu mada husika ambayo chapisho lako linafanya vizuri yaani inapata “Engagement – Likes, Comments, Share & Saves”
Kumbuka Insight unaangalia kwenye profile katika akaunti yako au unaenda kwenye setting kisha una click kwenye insight na utaweza kuona machapisho gani yanafanya vizuri, machapisho yako yamefikia watu wangapi, umepata followers wangapi na kujua muda mzuri wa kupost machapisho yako.
SOMA: KWANINI HAUPATI FOLLOWERS WA MAANA
#2 Tumia features pendwa kwenye Instagram story
Instagram story nakuwa nazungumzia poll features, question sticker, quiz sticker n.k ili kujua wafuasi wako wanapenda nini, kujua matatizo yao, kujua changamoto zao na matamanio yao na kujua ni aina gani ya maudhui yaani “Content”wanazipenda kwa kuauliza maswali, kwa mfano unauliza kati chai na kahawa wanapenda nini kupitia poll ya “Yes or No au “Ndio au Hapana” au “A au B” na utaweza kupata majibu ya wafuasi wako wanapenda nini.
Ni hivi…
Unatumia “Question sticker” kujua matatizo yao, kuwauliza maswali, kuwapa nafasi wafuasi wako kukuliza maswali na itafanya ujue changamoto zao na kutengeneza maudhui yenye kuendana na majibu ambayo upata kwenye Insta story yako.
Unatumia features mbalimbali kwenye Insta story itakusaidia kujua wafuasi wako wanapenda ili usiweze kuwapoteza katika akaunti yako ya instagram kwa kupost machapisho ambayo hawayahitaji ila wewe unadhani wanataka, hivyo penda kutazama sana insight sawa eeh!
#3 Andaa maudhui ambayo yanawavutia wafuasi walengwa
Umeshafanya utafiti na umebaini changamoto zao, matatizo yao, maumivu yao, matamanio yao maumivu yako na kitu gani kinawapa hamasa katika maisha yao, kwahiyo ukitengeneza maudhui kwa kugusa maeneo haya. Watakuwa tayari kukusikiliza kwa unawapa sababu ya kuendelea kuwepo katika akaunti yako ya Instagram.
Kama unasambaza yaani unashare maudhui ambayo hayawagusi wao na ndio itakuwa sababu ya ku-unfollow, kwahiyo hakikisha unatengeneza maudhui ambayo yanagusa kitu wanachopenda yaani Interest zao.
Kwahiyo…
Kabla ya kupost kitu chochote hebu jiulize…
Je, post inatatua tatizo la mtu?
Je, inazungumza na walengwa wangu ili wanunue bidhaa?
Je, inaungana na brand yaani chapa yako?
Je, inatatua changamoto ya mtu (Mfuasi wako)?
Kabla ya kuendelea…
Hakikisha unajibu maswali haya na ukipata jibu ndiyo basi post chapisho lako na wewe kaa pale unaona followers wako wanaongeka yaani Boom…! Na kupata kuona akaunti yako wafuasi wanaongezeka na machapisho yako kufanya vizuri. Hivyo andaa maudhui ambayo yanavutia walengwa wako katika akaunti ya Instagram yako.
SOMA: IDEA 11 ZA REELS KWA AKAUNTI YA BIASHARA INSTAGRAM
#4 Sambaza maudhui yako kwa fomati mbalimbali za post
Kuna fomati mbalimbali za kupost kwenye Instagram za kushare maudhui ambazo zipo kwa ajili yako wewe mfanyabiashara au unayetaka kuwa na ushawishi katika akaunti ya Instagram yako.
Unaweza kushare video fupi yenye sekunde tano hadi sekunde tisini ambazo unaweza kuweka picha, sauti, muziki au maandishi na hii inaitwa Instagram reel na uzuri reel inaweza kuwafikia watu wengi hata ambao hata hawafollow akaunti yako, anza kutumia itafanya upate wafuasi wengi wapya.
Unaweza kusambaza post za kupangusa yaani Carousel post ambao unaweza kupost picha kumi kwa wakati mmoja ni wafuasi wako kupangusa kwenda kushoto na kujifunza juu ya mada husika ni wewe kutoa thamani na kuzipangilia vizuri tu na hii inafanya upate wafuasi wapya na kuwatunza ambao unao.
Unaweza kusambaza post ya picha moja yaani Organic post au Single post ambapo unaweza kuweka picha na ujumbe au picha kisha chini unaandika caption ambayo inaelezea juu ya picha na kutoa value kwa kuelezea faida au ni kwa namna gani wafuasi wako wapata majibu ya matatizo na changamoto zao.
Share Instagram story na ukapost maisha yako ya kila siku, behind of scene ya kitu unachofanya na pia unaweza ku-pin katika highlight kwenye profile yako ili watu waweze kuona na uweze kuweka hali ya mamlaka yaani “Authority” katika akaunti yako.
Tumia Instagram Live kwa kuingia live na wafuasi wako kukuna unaongea juu ya mada fulani, kungumza na wafuasi wako, kupiga sori moja, mbili na kuonyesha mirejesho ya watu wakitumia bidhaa au huduma yako. Je, wewe unaingia Insta live kuungana na wafuasi wako?
Fanya matangazo yaani Sponsored Ads kusambaza maudhui yako kwa watu wengi ambao ni wafuasi wako na wale ambao si wafuasi wako ili waone chapisho lako na kuchukua hatua ya juu ya kile ambacho wewe umepost.
SOMA: JINSI YA KUPATA FOLLOWERS KWA KUFANYA COLLABO
#5 Ungana na page zenye walengwa wako
Instagram kuna watu walianza kabla yako na ni page nzuri sana na zina wafuasi wengi ambao unaweza kuwatoa katika page hizo na kuja kuwa wafuasi wako katika akaunti yako. Kwa sababu kuna page zinafanya vizuri na kuweza kuona wafuasi wao wanapenda nini, zimepata kuwa na ushawishi na watu wanaunga na kuacha comment, wanashare na wajibiana comment.
Ni hivi…
Ungana na page ambao umelenga kupata wafuasi wa maana kwa kuweka “Turn on notification” kwa kuona chapisho jipya kisha unasoma na kuweka comment nzuri kulingana page ya mtu amabye ume-follow page yake kwa kuandika comment ambayo inatoa thamani yani “add the value” na hata mtu akisoma comment aseme wow! Wewe ni mtu smart na aweza ku-click na kufungua profile yako…
Kwahiyo hakikisha bio yako inaeleza nini hasa unafanya, highlight zimepangwa vizuri, mpangilio wa post zao unavutia na rangi ya brand yako aseme huyu ndiye mwenyewe hahaha! Unacheka ni suala ya ku-follow ukurasa wako
Acha comment nzuri na sio zile comment “Naomba ufollow ukurasa wangu” basi kwa kujitangaza hivyo wewe utaonekana unalialia na una njaa. Kwahiyo weka comment nzuri ambayo inatoa thamani kwenye page na inakuonyesha wewe ni mtaalamu ambaye unajua nini unafanya kwenye mtandao wa Instagram.
#6 Tengeneza brand ambayo wafuasi wako walengwa wanapenda kuungana nayo
Brand sio logo kuonekana nzuri, graphic design nzuri badala yak brand ni pale wafuasi wako wanajisikiaje wanapokuwa wanaungana na ukurasa wako katika kitu unachofanya, kwa mfano chapa yako binafsi yaani “Personal brand” wafuasi wako wanasema nini wakati ambao wewe hao na wanajiskiaje wakiwa kwenye akaunti yako”.
Tengeneza brand ambayo watu wanapenda kuungana nayo na masuala ya logo, graphic design ni utambulisho wa chapa yako yaani “Brand Identity” ya brand yako,. Watu wajisikie wanaenda kutatua matataizo yao kwa wewe kujua ujuzi wako, una uzoefu gani, umesimamia wapi na hii inakupa mamlaka kwenye kitu unachofanya..
Tambua wafuasi wanataka nini na itafanya kuongeza followers wengi na ukurasa kukua siku hadi siku.
Je, umepaata kitu kwa kujifunza kwenye makala hii? Basi andika maoni yako ndani ya sekunde 60 nitakuwa nimekujibu bila ya kusahau uungwana ni kushare maudhui haya kwa watu ambao unataka wawe na ushawishi kwenye mtandao wa Instagram kwa kusambaza link ya blogu hii.