Je umekuwa ukichoshwa na kujaribu kuuza kwa kila mtu kwenye mitandao ya kijamii bila mafanikio?
Kwenye makala hii utakwenda kujua njia za kumvuta mteja mtandaoni na kubadilisha mtazamo wako juu ya biashara au chapa yako kwenye mitandao ya kijamii
Njia 5 za kumvuta mteja mlengwa mtandaoni
1. Tambua unataka kumvutia nani
Kama hujui unauza bidhaa au huduma yako kwa ajili ya nini, itakuwa ni ngumu kwako kuuza kwenye mitandao ya kijamii iliyo na kelele nyingi ambazo zitakusababisha kupoteza muelekeo na matumaini ya kile unachokifanya. Haya sasa jiulize maswali haya unataka kumvutia nani kwenye bidhaa au huduma yako? Wanapatikana wapi? Jinsia gani na umri wao vipi? Je wanapitia changamoto na maumivu gani ambayo bidhaa au huduma yakoinaweza ikawa ni suluhisho kwao?
Mfano wangu!
Wakina mama wenye umri kati ya miaka 25 – 45 walioolewa na wanaofanya kazi za ofisini katika mkoa wa Dar es salaam, wenye matatizo ya maumivu ya mgogo, miguu na uchovu baada ya kazi.
2. Wachunguze walengwa wako
Je walengwa unataka kuwavuta ili waje wanunue bidhaa au huduma yako, wanapitia changamoto gani, maumivu, matamanio na wanafikiria nini? Kama uliona nimeandika mfano kwenye njia ya kwanza njia ya pili inaweza ikawa hivi baada ya kujua unataka kumvutia nani
Wanaohitaji kuondoa uchovu ili waweze kuwahudumia watoto wao vizuri pindi wanaporudi nyumbani au ili kudumisha mahusiano yao na waume zao!
3. Chagua mtandao wanaopatikana
Jukumu lako kama mfanyabiashara au mtu unayetafuta pesa mtandaoni ni kuwa kwenye mitandao ya kijamii ambayo walengwa wako na watu wanokuingizia pesa au kufaidika na huduma au bidhaa zako wanapatikana. Je ni wapi wanapoteza muda wao baada ya kazi?
Wamefuata(follow) kurasa zipi kwenye mtandao wao pendwa? Wanapenda kutazama maudhui ya aina gani wakiwa kwenye huo mtandao? Ukishajua hayo ni muhimu kuanza kuwa active kwenye huo mtandao ili watambue uwepo wako.
4. Tengeneza maudhui yanayogusa matatizo na matamanio yao
Tayari umeshajua nini hakiwapi furaha na kipi huwapa furaha, sasa ni jukumu lako kuonyesha unawaelewa ili iwe rahisi wao kukujua, kukupenda, na kujenga uaminifu kwenye bidhaa au huduma yako ili watoe pesa mifukoni kwao uwatatulie changamoto au maumivu walionayo na kufikia matamanio yao(matokeeo mazuri)
Mfano njia rahisi za kuwa mchangamfu kwa watoto wako baada ya kazi!
5. Fanya matangazo ya kulipia kuwafikia wengine wasiojua kuhusu biashara yako
Moja wa kitu nachopenda kwenye matangazo ya kulipia ya facebook pamoja na instagram ni uwezo wa wewe kuwa Mbeya au mkoa mwengine na kufanya matangazo na kuwalenga watu wenye tabia au wanaopenda vitu fulani kwenye mitandao ya kijamii na waopatikana mkoa fulani ukitumia bajeti ndogo tofauti na ukiaenda kujitangaza kwenye Televisheni na Redio au kuweka matangazo barabarani
Kwenye mitandao ya kijamii ni llazima utumie pesa upate pesa, ukisema ooh mimi nina bidhaa au huduma nzuri na unakaa usubiriee watu wakutafute utaambulia patupu na biashara yako haitakua inavyopaswa. Kwahio kufanya matangazo ya kulipia ni muhimu. Sababu 3 kwanini utumie facebook ads 2022
Hitimisho
Kama unahitaji kuvutia wengi walengwa kwenye mitandao ya kijamii ni muhimu kujiweka kitaalamu ili unaowalenga wajue unawaelewa na wewe ndio mtatuzi wa matatizo na changamoto zao, hapo utafanikiwa kwenye biashara yako kwenye mitandao ya kijamii